makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Novemba, 2016
Serikali ya Ethiopia Yamshikilia Mwanablogu wa Zone9 Befeqadu Hailu kwa Kigezo cha ‘Hali ya Hatari’
Hailu alitarifiwa kuwa kukamatwa kwake kulisababishwa na mahojiano aliyoyafanya na Idhaa ya Amerika katika lugha ya Kiamfariki kuhusu hali ya hatari iliyotangazwa nchini Ethiopia.
Hofu ya Mkono wa Sheria? Kujitafutia Uhuru? Raia wa Gambia Wahoji Nchi yao Kujiondoa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai
"Kikwazo!! #Gambia yajiondoa ICC. Hii ni kutokana na hofu ya dikteta kwamba waziri wake wa ndani wa zamani atamponza katika kupata hifadhi"
Mazungumzo ya GV: Hisia Zetu Siku Sita Kabla ya Uchaguzi wa Marekani
Tukiwa tumebakiza siku sita kabla ya uchaguzi na kabla ya kumalizika kwa minyukano ya kampeni, kila mmoja anaisubiria siku ya uchaguzi kwa bashasha.
Morocco Yaondoa Vikwazo Dhidi ya Vitumizi vya VoIP Kuelekea Kongamano la Tabia Nchi la Umoja wa Mataifa.
"Ili kukwepa kuonekana kama ni nchi ya mabavu wakati wa kongamano la tabia nchi #COP22, nchi ya Morocco imerejesha kwa muda huduma za VoIP," alitwiti mtuaji mmoja wa mtandao wa intaneti.