makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Julai, 2014
Mkataba Uliovuja Waonyesha Hali Halisi Inayoikabili Sekta ya Gesi Nchini Tanzania

Kuvuja kwa mkataba kati ya kampuni ya Norway, statoil na serikali ya Tanzania waonesha hali ya mashaka kuhusiana na suala la mapato kwenye uvunaji wa gesi nchini Tanzania na suala la nani kunufaika na mkataba huo
Miezi Michache Baada ya Kupotea kwa MH370, Kuanguka kwa Ndege Nchini Ukraine Kwawashitua Raia wa Malasia
Mhudumu wa ndege wa Malaysia aelezea katika Instagram na Twita kuhusiana na watu wengi kupoteza maisha katika matukio ya ajali za ndege za Malaysia: "Katika kipindi cha miezi minne niliwapoteza marafiki zangu takribani 30."
Mwanamke wa Ivory Cost Aangushwa Kutoka Ghorofa ya Sita kwa Kudai Mishahara yake
Msichana mwenye asili ya Ivory Coast alipoteza maisha kutokana na kile kilichotaarifiwa kuwa alisukumwa na mwajiri wake na kuanguka kutoka ghorofa ya 6 ya jengo kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni ugomvi baina yao kuhusiana na malipo ya mshahara wa msichana huyo.
Baada ya Kuchoshwa na Kudorora kwa Uchumi, Wa-Ghana Waanzisha Harakati
Hali ya ghadhabu dhidi ya serikali ilitokana na ongezeko la haraka la kushuka kwa thamani ya fedha ya Ghana pamoja na kukosekana kwa mafuta vituoni hali iliyopelekea kuwa na misururu mikubwa ya watu katika vituo vya mafuta ya petroli
Mjadala Kuhusu Upatikanaji wa Mtandao wa Intaneti Wazidi Kushika Kasi Nchini Cuba
Raia wa nchini Cuba waendelea kudai kupunguzwa kwa gharama za mtandao wa intaneti pamoja na urahisi wa upatikanaji wake.