I am a Tanzanian, professionally a science Teacher specifically for chemistry and Mathematics. I fluently speak Kiswahili. As a Swahili speaker, its my duty to inform swahili speakers around the Globe with news which are hardly found in other news media but only in Global Voices, “Sauti za Dunia, Ulimwengu unaongea, wasikiliza”.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Disemba, 2012
Ni Sikukuu ya Kuzaliwa Kristo (Noeli) Mjini Betlehemu
Ni sikukuu ya kuzaliwa Kristo mjini Betlehemu, katika ukanda wa Magharibi, Palestina, mahali alipozaliwa Yesu Kristo. Ni namna gani nzuri ya kusherehekea tukio hili zaidi ya kuwashirikisha picha na maoni mbalimbali ya watumiaji wa mtandao wa intaneti kuhusiana na tukio hili linalosherehekewa na mabilioni ya watu duniani kote.
Mwanablogu wa Iran Sattar Beheshti Ateswa hadi Kufa
Watumiaji wa mtandao wa intaneti nchini Iran wameanzisha vurugu kubwa mtandaoni mara baada ya kupata habari ya kusikitisha ya kifo cha mwanablogu aliyefia rumande iliyowekwa mtandaoni kwa mara ya kwanza katika tovuti za upinzani. Sattar Beheshti alikamatwa mnamo tarehe 28, Oktoba 2012 na ilitangazwa kuwa amefariki takribani siku kumi baadae.