makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Mei, 2013
Hotuba ya Obama kwenye Mahafali Yaibua Mjadala wa Maana ya Uraia
Hotuba iliyotolewa wiki iliyopita na Rais wa Marekani Barack Obama kuhusiana na tafsiri ya uraia ilizua mijadala kadha wa kadha katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini China.
Mwanamke Aokolewa Kwenye Kifusi Baada ya Siku 17
Siku ifananayo na ile iliyogharimu maisha ya watu mara baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa tisa huko Savar pembezoni mwa mji mkuu wa Banglasesh, Dhaka, idadi ya watu waliofariki imeongezeka hadi 1,055 , idadi inayopelekea tukio hili kuwa tukio lililowahi kuua watu wengi zaidi tokea lile la tarehe 9/11 kulipotokea mashambulizi ya kigaidi, mfanyakazi mwanamke ajulikanaye kwa jina la Reshma Begum amekutwa akiwa hai mara baada ya kuzuiwa na kifusi cha jengo hilo kwa siku 17.
Pakistan: Imran Khan Aanguka na Kuumia Akiwa Kwenye Jukwaa la Kampeni
Aliyekuwa mchezaji maarufu wa kriketi na kisha kuamua kuwa mwanasiasa, ambaye kampeni yake ina tumaini kubwa la kuleta "Pakistan Mpya" aliyeweza kushawishi idadi kubwa ya vijana pamoja na wapiga kura wanaotokea mijini katika mikutano yake, alivunjika vifupa vitatu vya uti wa mgongo pamoja na mbavu baada ya kuanguka kutoka kwenye winchi iliyokuwa katika kimo cha futi 15 mda mfupi kabla ya kuhutubia. tukio hili limeonekana kuliunganisha tena taifa hili lililojigawa kwa visasi vinavyotokana na uchaguzi utakaofanyika mapema wiki hii.
Bangladesh: Waislamu Wadai Wanawake Wabaki Majumbani
Wanachama wa kikundi chenye msimamo mkali cha Kiislamu nchini kimewashambulia wanahabari wa kike waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kiuandishi wakati kikundi hicho kilipokuwa kikifanya maandamano katika jiji la Dakar kudai kutumika kwa sheria kali za kiislamu, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku wanawake kuchanganyika na wanaume. Mpaka madai yao yatakapotekelezwa, chama hicho kimejiapiza kulitenga jiji la Dhaka na sehemu nyingine za nchi hiyo ifikapo Mei 5, 2013 kwa kuwaweka wanaharakati wake katika maeneo sita ya kuingilia jiji hilo.
Wabunge wa Ukraine Wataka Utoaji Mimba Upigwe Marufuku Kisheria
Mapema mwezi Aprili, Wabunge watatu kutoka kambi ya Upinzani iitwayo“Svoboda” walipeleka mswada bungeni wenye lengo la kupiga marufuku utoaji mimba nchini Ukraine. Tetyana Bohdanova anataarifu mwitikio wa watumiaji wa mtandao kufuatia hatua hii ya Bunge la Ukraine.