makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Novemba, 2015
Global Voices Yashikamana na Watetezi wa Uhuru wa Kujieleza nchini Morocco
Jamii ya Global Voices yataka kutendeka kwa haki dhidi ya watetezi saba wa uhuru wa kujieleza wanaoshitakiwa nchini Morocco kwa makosa ya “kuhatarisha usalama wa ndani wa Taifa.”
Jamii ya Lumad Nchini Ufilipino Yasimama Kidete dhidi ya Uonevu
“Jeshi la Ufilipino liliharibu shule yetu. Pia, lilichoma majengo ya ushirika wetu wa kilimo. Nilijikuta nimefungwa gerezani na sasa nimeshitakiwa kwa kusingiziwa kosa la utekaji. Tuna hamu ya kuipata tena ardhi yetu tuliyoirithi kutoka kwa mababu zetu."
Michoro Yaonesha Harakati za Raia wa Ufilipino Wakipambana na Ukandamizaji
Nchi ya Ufilipino ina idadi ya raia wazawa wanaokadiriwa kufikia milioni 14. Wengi wa raia hawa wanaoishi maeneo ya vijijini wapo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na uharibifu unaotokana na shughuli za uchimbaji madini, harakati za utafutaji maendeleo pamoja na matumizi ya nguvu za kijeshi.
Wanablogu wa Zone9 Wasema, ‘Kushikiliwa kwetu Kumefunua Yaliyojificha Nchi Ethiopia’
"Kwa wale waliotufunga gerezani na ambao walitusababishia madhila haya, hata kama hautuombi msamaha, sisi hatuna kinyongo."