I am a Tanzanian, professionally a science Teacher specifically for chemistry and Mathematics. I fluently speak Kiswahili. As a Swahili speaker, its my duty to inform swahili speakers around the Globe with news which are hardly found in other news media but only in Global Voices, “Sauti za Dunia, Ulimwengu unaongea, wasikiliza”.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Juni, 2014
Wanajumuia wa Global Voices Washinda Tuzo za Knight News Challenge za Kuboresha Huduma ya Intaneti
Katika matokeo yaliyotangazwa hivi leo, wanajumuia wawili wa Global Voices waibuka washindi wa shindano la mwaka 2014 la Knight News Challenge.
Uhamaji wa Watoto Wachukuliwa kuwa ni Baa la Kibinadamu
Kutoka Mexico, Katia D'Artigues, ambaye ni mwandishi wa blogu ya Campos Elíseos (Champs Elysées), aandika kuhusiana na watoto kulazimika kuhama wao wenyewe [es], hali inayompelekea kuiita hali hii kuwa ni “baa la kibinadamu”: Son niños que son orillados a cruzar la frontera solos. No lo hacen por aventura, sino porque...
Watoto Wachanga 44,000 wa Madagaska Hupoteza Maisha kila Mwaka kwa Kukosa Matunzo. Tunawezaje Kukabiliana na Hali Hii?
Huduma ya afya kwa watoto nchini Madagaska hairidhishi kabisa, lakini baadhi ya mashirika yanajituma kwa kadiri ya inavyowezekana ili kukabiliana na tatizo hili la kusikitisha.
Salamu, Brazil: Mashabiki wa Kiislam wa Kandanda na Kombe la Dunia la FIFA
Raia wa Colombia aliye na makazi yake katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Marcelino Torrecilla anatuhabarisha [es] kuhusiana na upekee wa mashabiki wa kiislamu wa mpira wa miguu kwenye Kombe la Dunia la FIFA, 2014 : Katika Kombe la dunia, waislamu 50,000 wamesili kutoka katika mataifa mbalimbali kama vile Irani,...
Maandamano Makubwa Yafanyika huko Guangzhou, China
Mamia ya wakazi wa Guangzhou jana mchana walikusanyika huko Sanyuanli kupinga hatua ya polisi ya kutaifisha mali binafsi za watu kwenye bohari kama sehemu ya harakati za kukabiliana na majanga ya moto. Waandamanaji walijikuta wakikabiliana vikali na polisi, na baadae, wakati wa vurugu hizo, waandamanaji walifikia hatua ya kupindua magari...