Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Machi, 2014
Mazungumzo ya GV: Namna ya Kutengeneza Video za Utetezi na Mabadiliko
Je, unatumia video kuifanya kampeni kuwa uhalisia? Je, una mpango wa kusimulia habari zako kwa kutumia kamera -au simu yako? Basi unahitaji kutazama video hii ya Mazungumzo ya GV!
Watumiaji wa Huduma ya Tor Waongezeka Nchini Uturuki
Mtetezi wa haki za binadamu na maadili Frederic Jacobs anabainisha kuwa idadi ya watu wanaotumia huduma ya Tor imeongezeka nchini Uturuki: Matumizi ya huduma ya Tor yako juu. Watu. > 35...
Erdogan Aapa “Kuifutilia Mbali” Twita Nchini Uturuki
Uturuki imeufunga mtandao wa Twita -sambamba na huduma ya Google ya DSN, ilitumika kupata huduma hiyo ikiwa imefungwa. Inaonekana, hata hivyo, kuwa mpango wa serikali ya Uturuki wa kudhibiti watu unakutana na mipango mbadala ya raia kuendelea kutwiti.
Mwanablogu wa Misri Alaa Abdel Fattah Aachiwa kwa Dhamana
Furaha imeendelea kutawala wakati mwanablogu maarufu wa Misri Alaa Abdel Fattah ameachiwa kutoka jela. Kwenye twiti yake ya kwanzabaada ya kuachiliwa, mwanaharakati huyo anaapa 'kuendeleza' mapambano.
Mazungumzo ya GV: Namna ya kushinda Ufadhili wa Miradi Midogo ya Rising Voices
Je, unalo wazo la kuisaidia jamii yako kusimulia habari zao kupitia mitandao ya kijamii? Kwenye Mazungumzo ya GV timu ya Mradi wa Rising Voices inajadili namna bora ya kushinda shindano la ufadhili wa miradi midogo
Maandamano ya Taiwan ya #KupingaBunge, Yatafsiriwa
Mamia ya watafsiri wamejipanga kupitia mtandao wa facebook kutafsiri habari kuhusu maandamano ya raia wanaojikusanya kwenye Bunge la nchi hiyo kupinga hatua ya chama tawala nchini humo kupitisha mkataba wa kibiashara wenye utata na nchi ya China.
Namna 10 Ambazo Warusi na Wa-Ukraine Walivyopokea Hotuba ya Putin Kuichukua Crimea
Vyovote mtu anavyojisikia kuhusu suala la Crimea, hotuba [ya Putin], ilikuwa ya kihistoria, na ndiyo ambayo wanablogu waliipokea kwa gumzo, kama ilivyo kawaida yao mtandaoni.
Msichana Nchini Madagaska Ajiua Baada ya Picha Zake Kusambazwa Facebook
Koolsaina anaandika kwamba msichana mmoja wa ki-Malagasi alijiua [fr] baada ya picha zake kusambazwa kwenye ukurasa wa Facebook unaoonyesha picha za wasichana wa Madagaska bila ruhusa yao. Wito ulitolewa kwa...
Mazungumzo ya GV: Heri ya Miaka 25 ya Kuzaliwa, Mtandao!
Kuna tofauti gani kati ya Intaneti na Mtandao? Kwa nini mtandao wazi ni muhimu? Jopo la wataalamu maarufu wa teknolojia na watetezi wa haki wanazungumzia hilo kwenye Mazungumzao ya GV.
Maandishi ya Facebook Kukosoa Kuivamia Crimea Yamgharimu Mwandishi Ajira
Warusi wanauliza ikiwa Putin anaweza kwenda "kuwavamia" na wao, kama hiyo inamaanisha kuongeza mafungu ya fedha kwa ajili ya majimbo yaliyosahaliwa