Machi 18, 2014, siku mbili baada ya wa-Crimea kupga kura ya maoni kuamua kujiunga na Shirikisho la Urusi, Rais Vladimir Putin alitoa hotuba [ru] akitangaza kuwa ameipokea Crimea na mji wa bandari ya Sevastopol kuwa wanachama wapya wa shirikisho hilo. Mpaka wakati tangazo hilo linatolewa, haikuwa wazi ikiwa Urusi itarekebisha mipaka ya nchi hiyo mara moja, au itawaacha wanachama ao wapya kuwa huru kama zilivyo Abkhazia, South Ossetia, au Transnistria.
Pamoja na namna yoyote ambayo mtu anaweza kujisikia kuhusu suala la Crimea, hotuba hiyo ilikuwa ya kihistoria, na ambayo wanablogu waliiipokea kama kawaida ya mijadala ya mtandaoni. Hapa ni baadhi ya mijadala hiyo:
1.
Warusi wengi waliipokea kwa furaha. Zaidi ya yote, hata kwa mujibu wa kura za maoni za upinzani [ru] wengi wanaunga mkono “kutwaliwa kwa mara nyingine” kwa eneo hilo.
2.
Kwa wengine, hisia zilikuwa mchanganyiko. Ikiwa Putin “ameiiba” Crimea, je bado litakuwa jambo jema? Labda ni mtindo mpya, kama mchezo wa video.
3.
Ungeweza kumtegemea Waziri Mkuu Dmitry Medvedev kuweka mambo katika hali ya utulivu na angalau kutoa maelezo. Kulala kwake wakati wa shughuli za hadharani imekuwa kawaida katika miezi ya hivi karibuni ambapo Urusi inatengeneza sera.
4.
“Kuanzia leo ninaachana na bidhaa za kimarekani maishani mwangu. Marafiki, niungeni mkono!” alitwiti Mikhail Dvorkovich, mfanyabiahsra wa Kirusi na kaka wa mshauri wa Medvedev, ikiwa ni majibu kwa tishio la Marekani kuweka vikwazo[Ripoti ya Global Voices] dhidi ya maafisa wa Urusi. Watu wengi walijadili ujasiri wa kutwiti kwa kutumia simu ya iPhone, na, kwa hakika, kwa kutumia huduma iliyoanzishwa marekani ili kuwafikia aliotaka wasikie anachosema.
5.
Baadhi ya wanablogu wa ki-Rusi wanaonekana kuviangalia vikwazo dhaifu vya Marekani kama dalili ya kuunga mkono kimyakimya matendo ya Rais Putin. Huenda ndio sababu ya picha yake hii nyeti ya kutengeneza ikimwonyesha akiwa katika magwanda ya Idara ya Usalama wa Taifa la Urusi. “Asante sana comrade Obama!”
6.
Kwa upande mwingine, Waukraine wanaonekana kusikitishwa sana na hotuba ya Rais Putin. Mwitikio kama huu unaonekana kuonyesha hisia hizo.7.
Kulinganisha hatua hiyo na ile ya kundi la Nazi imekuwa kawaida ya mijadala ya kishabiki baina ya Warusi na Waukraine kwa miezi kadhaa sasa, na sasa, hali haijabadilika.
8.
Na hata tendo la hisani lakufananishwa na kundi la Nazi, kama hilo linawezekana.
9.
Picha ya kijana wa Caucasia Kaskazini akicheza kwenye mitaa ya Urusi. “Kama hutakuwa mwangalifu, Crimea,” anasema aliyeipiga picha hiyo, “mtageuka kundi la wachache wanaonyanyasika Urusi!” Haya ndiyo mategemeo ya wote wanaoshutumu hatua hiyo inayolinganishwa na ile ya U-Nazi.
10.
Baadhi ya Waukraine wamebaki na matumaini kuwa Marekani na Umoja wa Ulaya watachukua hatua madhubuti kumwadhibu Putin na Urusi yake. Na kama Shirikisho la Urusi litatimuliwa kwenye kundi la G8 mwaka huu, nani achukue nafasi hiyo mwingine zaidi ya Ukraine?