· Novemba, 2009

Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Novemba, 2009

Irani: Vuguvugu la Kijani Laupinga Utawala Tena

Upande wa upinzani wa Vuguvugu la Kijani nchini Irani mnamo tarehe 4 Novemba uliendesha maandamano makubwa ambapo maandamano hayo yalikabiliwa na matumizi makubwa ya nguvu ya kuyazuia yaliyofanywa na vikosi vya usalma. Kama ambavyo sasa inatarajiwa, uandishi wa habari wa kiraia nchini Irani haukukosa kitu kwani ulirekodi 'historia' hiyo kupitia simu zao za mikononi.

6 Novemba 2009

Kutambulisha Sauti Zinazotishwa

Leo, kitengo cha utetezi cha Global Voices, kinazindua tovuti mpya inayoitwa Threatened Voices, yaani, Sauti Zinazotishwa ili kusaidia kufuatilia unyamazishaji wa uhuru wa kujieleza wa mtandaoni. Inaonyesha ramani ya dunia na mwingiliano wa saa unaosaidia kuonyesha taarifa za vitisho na ukamataji unaofanywa dhidi ya wanablogu duniani kote, na ni mhimili mkuu wa kukusanyia taarifa kutoka katika asasi na wanaharakati walioamua kujitoa muhanga kwelikweli.

6 Novemba 2009

Misri: Watu 10 Wenye Ushawishi Zaidi Nchini

Mtoto wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak, anayitwa Gamal Mubarak, -- na ambaye anatarajiwa kumrithi baba yake nafasi hiyo -- aliibuka kama mmoja wa washindi 100 wa TIME. Wanablogu wa Ki-Misri wana ya kueleza kuhusu jambo hili.

4 Novemba 2009