Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Aprili, 2012
Senegali:Rais Wade Aandamwa Hata Baada ya Kukubali Kushindwa Uchaguzi
Wakati nchi nyingine zikionekana kushangilia "uungwana" wa Bbdoulaye Wade kukubali matokeo nchini Senegali, wanablogu wa nchi hiyo bado wamemkaba koo Wade kwa kuushambulia Urais wake wakikumbushana ghasia za kuelekea uchaguzi, kubinywa kwa uhuru wa habari na mifano mingi ya utawala mbovu.
Bolivia: Wanaharakati Washinikiza Upatikanaji Nafuu wa Mtandao wa Intaneti
Nchini Bolivia, kuunganishwa na mtandao wa intaneti ni miongoni mwa huduma ghali zaidi duniani. Huduma hiyo haina kasi na bado haijaweza kupatikana kwa idadi kubwa ya watu. Kikundi cha wanaharakati kwa kutumia mtandao na nje ya mtandao kinadai huduma nafuu na bora zaidi.
Tunisia: Miitikio Tofauti Kufuatia Kuingiliwa kwa Barua Pepe za Waziri Mkuu
Mnamo Aprili 8 “Anonymous Tunisia” kikundi kisichotambulisha majina ya wanachama wao nchini Tunisia (ambacho kinadai kuwa na uhusiano na kikundi cha watu “wasiojitambulisha” ) waingiliao mawasiliano ya watu kiliingilia mawasiliano the ya barua pepe ya waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali. Vuguvugu hilo lilipewa jina la utani la (“Achana na Tunisia yangu”) ambayo ni sehemu ya kampeni kuu iitwayo “Operesheni Rejeza Tunisia”.
Uganda: Ndiyo Tunampinga Kony!
Kampeni kwenye mitandao ya kijamii inayokusudia kuongeza uungwaji mkono wa harakati za kumkamata kiongozi wa waasi wa ki-Ganda na mhalifu anayetafutwa kwa udi na uvumba Joseph Kony imechukua sura nyingine.
Mali: Kimya cha Wanablogu wa Nchini Humo
Wakati mtandao wa intaneti umetawaliwa na blogu, ujumbe wa twita na video kutoka nchi mbalimbali, watumiaji wa intaneti wenyeji wa Mali wangali kimya. Mji mkuu, Bamako, umeathirika kwa kukatika kwa umeme kwa kile kinachodaiwa kuwa kuadimika kwa mafuta. Katika mazingira kama haya, kipaumbele si kutuma ujumbe, bali kutafuta kutafuta taarifa kuhusu viongozi wapya wa sehemu ya Kaskazini ya Nchi hiyo.
Ghana: Matumizi ya Vyombo vya Habari vya Kiraia katika Uchaguzi wa Mwaka 2012
Wananchi wa Ghana wanajitayarisha kwa ajili ya uchaguzi wa rais na wabunge ambao utafanyika tarehe 7 Disemba 2012, Jumuiya ya wanablogu wa Ghana imezindua mradi wa uanahabari wa kijamii ambao una nia ya kufunza wanaharakati, vikundi vya kisiasa na wanafunzi kutumia zana za uanahabari wa kijamii kwa ajili ya kwa ajili ya kuafuatilia na kuripoti shughuli za uchaguzi.