Uganda: Ndiyo Tunampinga Kony!

Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu zaKony 2012.


Kampeni kwenye mitandao ya kijamii
inayokusudia kuongeza uungwaji mkono wa harakati za kumkamata kiongozi wa waasi wa ki-Ganda na mhalifu anayetafutwa kwa udi na uvumba Joseph Kony imechukua sura nyingine. Katika posti ya blogu iitwayo“#Kony2012 ni shairi”, Sean Jacobs anazitazama video hizo mashairi ya wimbo wa mtandaoni kuhusu kampeni hiyo inayosambaa kama moto wa nyika.

Shirika la habari za muziki wa kughani” a> la ki-Australia limekuja na kibao kingine kiitwacho “Ndiyo Tunashiriki kampeni dhidi ya Kony”:

NDIYO TUNAMPINGA KONY. Ni mwezi Machi, na mtandao unasambaza soga la kwanza duniani kote kwa mwaka 2012: video iliyozuilika ya Mzuie Kony 2012, inayoonyesha hali ngumu wanazokumbana nazo mtoto wa ki-Afrika anayechapa gwaride kwa namna ambayo haijapata kutokea. Lakini je, ni vyema kweli? Je, ni vibaya kweli? Au dunia ni ngumu kueleweka zaidi kuliko “watu wema” au “wabaya” wanavyoweza kueleweka? Vyovyote iwavyo; jambo moja ni la hakika na lenye umuhimu; kamwe haijawahi kutokea video ya dakika 27 isiyo na upuuzi na ujinga kusambaa namna hii. Je, hii ni kuonyesha uwezo wa mtandao kuwajulisha na kuwafanya mamilioni washiriki; na alama ya matumaini kwamba kuna utashi miongoni mwa mamilioni hao, na kwa shauku kabisa kujihusisha na kitu chenye maana kubwa? Au je, kampeni dhidi ya Kony 2012 inaashiria mwanzo wa enzi yenye msukumo mpya wa kusambaza habari zenye kuwanadi wanadamu? Jiunge na mwenyeji wetu wa kujitolea Robert Foster –na mgeni wetu maalum, General Bazter, mkurugenzi wa AFRICOM –kadri tunavyochimbua kiini halisi cha suala hilo.

Tony 2012 t-shirt. Image courtesy of http://www.districtlines.com/.

Fulana ya Tony 2012. Picha kwa hisani ya http://www.districtlines.com/.

Kikundi cha maaigizo kiitwacho Bath Boys Comedy kimeanzisha kampeni iitwayo Tony 2012: Mzuie Mnyama. Mnyama Tony ni katuni ya matangazo kwa ajili ya bidhaa ya vitafunwa vya Kellogg, inayoonekana kwenye vifuko na matangazo yake.

Kwa uwazi, Adolph Hitler aliitikia kampeni hiyo ya video ya Kony 2012:

Mtumiaji wa mtandao wa You TubeStabOfMyVenom has aliunganisha vichekesho muhimu vya Joseph Kony 2012:

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=jJIPl17csfw

Kampeni ya Kony 2012 imekosolewa vikali na wa-Ganda wengi wanaodai kwamba video hiyo inarahisisha mno mgogoro huo wa Kaskazini mwa Uganda. Ili kupingana na picha hasi ya Afrika kwenye video hiyo, raia watumiao mtandao wanatuma ujumbe kuhusu “kile wanachokipenda Afrika” kwa alama ya ujumbe #WhatILoveAboutAfrica.

Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu zaKony 2012.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.