Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Februari, 2011
Gabon: Wanafunzi Waandamana, Wanajeshi Wasambazwa
Mgogoro wa kisiasa nchini Gabon ulifikia vilele vipya siku ya Alhamisi, wakati wanafunzi walipoandamana katika Chuo Kikuuu cha Omar Bongo kilichopo ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo, Libreville. Wakati maandamano ya juma lililopita yalishirikisha zaidi wanachama wa vyama vya upinzani, mgogoro huu unaonekana kupelekea kuwa mgogoro mkubwa zaidi wa kijamii.