Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Aprili, 2015
VIDEO: Dunia Inasema #WanabloguZone9WaachiweHuru
Global Voices inakumbuka mwaka mmoja tangu kuwekwa kizuizini kwa wanablogu wa Ethiopia wa Zone9 kwa kutengeneza video hii ya kuwaunga mkono. Sema pamoja nasi: #WanabloguZone9WaachiweHuru!
Maisha ya Wakenya Yana Thamani, Wanafunzi wa Kiafrika Wasema Kwenye Ibada ya Kuwaombea Wahanga wa Garissa Jijini Beijing
Kikundi cha wanafunzi wa Kiafrika jijini Beijing waliandaa ibada ya kuwakumbuka wahanga 147 wa shambulio la Garissa pamoja na china kutokuwa na uvumilivu kwa watu wanaoomboleza hadharani
‘Msanii wa Uke’ Nchini Japani Akana Mashitaka ya Ukiukaji wa Maadili
Msanii wa Kijapani Megumi Igarashi, anayeitwa kwa jina la utani "Msanii wa uke" na vyombo vya habari vya Magharibi, anasema sanaa yake inayotokana na sehemu zake za siri haivunji maadili.
Mbali na Kusikia Habari za Boko Haram Nchini Niger, Fahamu Jangwa la Ténéré
Niger ipo katika vita na Boko Haram. Tusilisahau hili, hata hivyo, Niger ni mahali palipo na miradi mingi na pia ni eneo lililosheheni utajiri mwingi wa asili pamoja na ushairi.
Watu 147 Waliouawa Garissa Ni Zaidi ya Takwimu
Watumiaji wa mtandao wa Twita wameanza kutumia alama habari #147notjustanumber kuadhimisha maisha ya wahanga wa shambulio la kigaidi lililotokea kwenye Chuo Kikuu cha Garissa.