VIDEO: Dunia Inasema #WanabloguZone9WaachiweHuru

#FreeZone9bloggers kutoka Global Voices kwenye mtandao wa Vimeo.

Mnamo Aprili 25, 2014, wanablogu tisa wakiwemo waandishi wa habari waliwekwa kizuizini nchini Ethiopia. Baadhi yao walifanya kazi na blogu ya pamoja iitwayo Zone9 inayochambua masuala ya kijamii na kisiasa yanayoendelea nchini Ethiopia ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa wa haki za binadamu na uwajibikaji wa serikali kwa wananchi. Wanne wao walikuwa waandishi wa Global Voices. Mwezi Julai, walifunguliwa mashtaka chini ya sheria kupambana na ugaidi nchini humo. Wamekuwa kizuizini tangu wakati huo na bado wanangoja kuendeshwa kwa shauri lao.

Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa wanablogu wa Zone9, jumuiya yetu ilitengeneza video hii kuwaunga mkono ndugu zetu hawa wanaoshikiliwa jela. Mkusanyiko huu wa vipande vya video umebeba sauti zinazotaka haki itendeke kutoka nchi za Mexico, Chile, Marekani, Cuba, Croatia, Colombia, Kenya, Uholanzi, Iran, Syria, Ufaransa, Azerbaijan na bila shaka, Ethiopia. Tazama, sambaza, na sema pamoja nasi: #WanabloguZone9WaachieHuru!

Video hii ilitengenezwa na J. Tadeo, Elizabeth Rivera, Elaine Díaz, Lully Posada, Daudi Were, Angela Oduor Lungati, Sebastian Mitchell, Nekesa Were, Pauline Ratzé, Niki Korth, Leila Nachawati, Marie Boehner, Marinella Matejčić, Mahsa Alimardani, Arzu Geybullayeva, Endalk Chala, Ellery Roberts Biddle, na Sahar Habib Ghazi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.