‘Msanii wa Uke’ Nchini Japani Akana Mashitaka ya Ukiukaji wa Maadili

Megumi Igarashi, July 24, 2014, YouTube screen capture.

Megumi Igarashi, Julai 24, 2014, imetolewa kwenye video ya YouTube.

Msanii wa Japani Megumi Igarashi, anayefahamika kwa jina la utani “Msanii wa uke” na vyombo vya habari vya kimagharibi, anasema hakuna ukiukwaji wowote wa maadili kwenye kazi yake ya sanaa inayotumia sehemu zake za siri.

(Megumi Igarashi) alipoonekana kwa mara ya kwanza mahakamani, alikana mashitaka ya kukiuka maadili. (´-`).。oO (Ninafurahi sana msanii wa mahakama aliweza kumjengea taswira nzuri.  ー(^o^)

Polisi wa Jiji la Tokyo walimkamata Igarashi mwezi Julai 2014 kwa kudaiwa kuwatuma viungo vya mtandao kwa njia ya barua pepe kwa wafadhili wa mradi wake ili waweze kupakua (download) data zenye taswira halisi ambazo zingeweza kutumika kutengeneza kayak zenye sura ya uke inayotokana na sehemu zake za siri.

Igarashi alikamatwa tena mara kadhaa kwa kuonesha kazi yake ya sanaa iliyokuwa na sura ya sehemu zake za siri kwenye duka moja la ngono jijini Tokyo -kitendo cha kidhalilishaji kilichofanywa na Polisi, kwa mujibu wa mawanasheria wake.

Kwa miezi kadhaa kabla ya kukamatwa kwake mwezi Julai, Igarashi, anayetumia jina la ‘Rokudenashiko” ( ろくでなし子 yaani “msichana wa hovyo”), alipata umaarufu kwa kutengeneza aina mbalimbali za kazi ya sanaa kwa kutumia sura ya sehemu zake za siri.

Megumi Igarashi, kwa jina jingine Rokudenaishiko, ni msanii wa Tokyo anayetuhumiwa kukiuka maadili. Hebu tuangalie baadhi ya kazi zake za sanaa.

Nchini Japan, vyombo vya habari kuonesha sehemu za siri ni kosa la jinai chini ya Kifungu cha 175 cha makosa ya jinai. Zuio hilo lilianza enzi za Meiji, wakati Japani ikianza kukubaliana na utamaduni na taasisi za kimagharibi kwenye nusu ya pili ya karne ya 19.

Hata hivyo, ibara ya 175 haina mwongozo uliowazi kwa polisi au mahakama kuhusu kile kinachoweza kuitwa kukosa maadili katika kesi kama hizi::

…Hakuna kifungu kwenye ibara hii, kinachotafsiri neno “ukosefu wa maadili” na “si watawala wa serikali wala mahakama zililazimishwa kufafanua kile kinachoitwa “vitu visivyo vya kimaadili. Inashangaza kidogo kwamba tafsiri nyingi zimekuwa zikitolewa kwenye ibara hii kuhusiana na namna inavyoweza kutumika. Kama tunachukulia vifaa vinavyoonekana kama vile manga au sinema, sheria imetafsiri neno ukosefu wa maadili kwenye ibara hii kama kuonesha vinyweleo vya sehemu za siri, sehemu za siri za watu wazima na tendo la ngono. Kwa hiyo, kama hili ndivyo lilivyo basi maana yake kifaa chochote kinachoonesha sehemu hizi lazima kifichwe kwa kile Japani inachokiita bokashi (giza giza/kivuli) au kwa ukungu wa kidijitali. Tafsiri hii ya uvunjifu wa maadili isiyo na maana inayoeleweka imesababisha kutokufanana kwa maamuzi mengi ya mahakama, ambavyo ni sehemu ya mjadala wa uhuru wa kujieleza nchini Japani.

Utamaduni wa Japani pia una mwiko mkali kuhusu kujadili au hata kuonesha kuwa kuna kiungo kinaitwa uke (ingawa Metroplis TV yenye Kidachi, mchapishaji wa kipande hiki kinachoelimisha hapa chini, haina tatizo na kutumia maneno kama “Mtumbwi wa uke” kuelezea kayak za Igarashi zenye sura ya uke):

Akipatwa na hatia, Igarashi anaweza kuhukumiwa mpaka miaka miwili jela na kutozwa faini inayfofikia yen 2.5 milioni (sawa na dola la Marekani 20,900).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.