Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Agosti, 2012
Brazil: Mtoto wa Miaka 13 Aonyesha Matatizo ya Shule Kupitia Facebook
Diário de Classe [pt], ukurasa wa Facebook uliofunguliwa na Isadora Faber, aliye na miaka 13 na anayetokea Santa Catarina, Brazil, tayari umeonyesha kupendwa zaidi ya mara 176,000. Huku lengo lake likiwa...
Sudani: Mwanaharakati Mtumia Twita Aachiwa Huru
'Nilitishiwa kufanyiwa vitendo vya ngono na kutendewa vibaya mara kadhaa katika siku ile. Wakati mmoja hata na ofisa wa ngazi za juu wa #NISS.' Mwezi Juni, Shirika la Ujasusi na Usalama wa Taifa la Sudani liliwakamata maelfu ikiwa ni pamoja na mwanaharakati anayetumia Twita Usamah Mohamed Ali.
Syria: Mafunzo ya Silaha na Namna ya Kupigana Katika Mtandao wa Intaneti
Waasi nchini Syria wameanza kutumia YouTube ili kupeana mafunzo hasa kupitia 'Free Syrian Army Help' yaani 'Msaada wa Jeshi la Kuikomboa Syria'. Chaneli hiyo ina picha za video zipatazo 80 zikiliezea mbinu kama vile vita ya uso-kwa-uso, jinsi ya kutengeneza mabomu ya kutupwa kwa mkono, na jinsi ya kuwavizia maadui.