Sudani: Mwanaharakati Mtumia Twita Aachiwa Huru

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalumu kuhusu Sudani Yaendesha Mapinduzi.

Shirika la Ujasusi na Usalama wa Taifa la Sudani (NISS) lilijimwaga mitaani na kuendesha kampeni kubwa ya kamatakamata, ambapo liliwakamata maelfu ya waandamanaji, wanaharakati, wanachama wa vyama vya upinzani vya kisiasa na viongozi na hata raia wanaoitii sheria waliokutwa maeneo ya maandamano, vyuo vikuu, maeneo ya umma na hata kwenye nyumba za watu, kufuatia maandamano ya kupinga utawala ulio madarakani yaliyoanza katikati ya mwezi Juni.

Hata hivyo, baada ya kutulia kwa maandamano hayo zaidi ya miezi miwili tangu yaanze #SudanRevolts, Shirika la Ujasusi limeanza kuwaachia mahabusu. Tarehe 17 Agosti, 2012, ilikuwa siku ambayo kwayo mahabusu wengi waliachiwa.

Miongoni mwa walioachiwa ni pamoja na mwanaharakati anayetumia Twita Usamah Mohamed Ali ambaye alikamatwa katika eneo la tukio la maandamano jijini Khartoum mnamo tarehe 22, 2012.

Usamah Mohamed Ali is a Sudanese Twitter activist who was arrested at a protest. He tweets his prison experience following his release

Usamah Mohamed Ali ni mwanaharakati wa nchini Sudani anayetumia Twita na ambaye alikamatwa wakati wa maandamano. Anatuma twiti kuhusu aliyoyaona gerezani baada ya kuachiwa kwake

Mwezi mmoja tangu kukamatwa kwa Usamah, Mimz aliandika makala kwenye bloguakizungumzia kutiwa kwake mahabusu.

Siku moja baada ya kuachiwa kwake, alituma twiti ya maneno mawili tu; lakini aliwathibitishia wafuasi wake kwamba alikuwa ameachiwa huru:

@simsimt: Mapambano yanaendelea.

Aliongeza:

@simsimt: Ninawashukuru sana wote walionitia moyo! Twiti, mada & amp; ujumbe wa kuungwa miono ulinitia donge kooni mara nyingi tu nilipokuwa nikizisoma!

Wiki moja baadaye, Usamah aliandika mfululizo wa twiti fupifupi akielezea hali iliyokuwepo wakati wa kukamatwa kwake.

Alianza kwa kusema:

@simsimt: Bila kutoa undani sana wa mambo kwa sasa, nilikamatwa na jasusi aliyekuwa kwenye mavazi ya kiraia wa #NISS ambaye alinifuata wakati nikiandika twiti. #SudanRevolts

na:

@simsimt: Nakumbuka wazi kabisa kwamba nilikuwa nikiandika kuhusu juhudi kubwa zilizofanywa na #NISS kuzuia ingizwaji kwenye rekodi wa aina yoyote wa maandamano hayo. #SudanRevolts

Usamah alieleza kwamba alikataa kutoa nywila (neno la siri) la simu yake, jambo lililowakasirisha maofisa wa Shirika la Ujasusi la NISS:

@simsimt: Kufunga simu yangu, ambayo inatumia nywila, baadaye ilikuja kuwa kichocheo cha kutendewa vibaya sana, kuteswa n.k.; mahojiano ambayo nimeyastahimili #SudanRevolts

akieleza:

@simsimt: Nilipopelekwa kwenye gari (pick up) la #NISS lililokuwa limeegeshwa katika eneo la maandamano, niliamriwa mara kadhaa kufungua simu yangu. #SudanRevolts

Na:

@simsimt: Nilikataa katakata. Baadaye waliamua kuachana nami, lakini baadaye walinipakia peke yangu kwenye gari lao hilo, huku wakiwa wamenifunga macho, hadi kwenye ofisi za #NISS huko Bahri. #SudanRevolts

Kisha anaeleza kuhusu mateso ya kihisia na kimwili aliyoyapitia wakati akiwa kizuizini:

@simsimt: Katika jengo la #NISS, nilistahimili karibu saa 4 au 5 za kutukanwa, kupigwa na vitisho vya kila aina ili tu nifungue simu yangu #SudanRevolts

Aliongeza:

@simsimt: Nilitishiwa kufanyiwa vitendo vya ngono, mara nyingi tu katika siku hiyo. Wakati fulani hadi na ofisa wa ngazi za juu wa #NISS. #SudanRevolts

Alieleza kwamba:

@simsimt: Nilistahimili vipigo vikali kichwani kwangu kwa jiwe, kwa sababu simu yangu waliyokuwa wanaishikilia ilipigiwa simu kutoka Marekani. #SudanRevolts

Na:

@simsimt: Mtesaji aliyekuwa sasa kama aliyechanganyikiwa alikuwa akitukana na kupaza sauti akisema “Wewe ni jasusi, JASUSI, JASUSI!” huku akinipa kipigo! #SudanRevolts

Alieleza kwamba maofisa wa NISS walihakikisha kwamba hapati hata lepe la usingizi:

@simsimt: Hadi hapo walipoamua kuachana na mimi, niliamrishwa na ofisa aliyekuwa mbele yangu, kunyimwa usingizi. #SudanRevolts

Usamah alihitimisha kwa kusema:

@simsimt: Ninaituhumu #NISS kwa kila jambo baya nililotendewa. Ninazikumbuka vizuri sura za watesi wangu na walionitembea vibaya. #SudanRevolts

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalumu kuhusu Sudani Yaendesha Mapinduzi.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.