Gabon: Wanafunzi Waandamana, Wanajeshi Wasambazwa

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum kuhusu Machafuko nchini Gabon 2011

Mgogoro wa kisiasa nchini Gabon ulifikia vilele vipya siku ya Alhamisi, wakati wanafunzi walipoandamana katika Chuo Kikuuu cha Omar Bongo kilichopo ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo, Libreville. Wakati maandamano ya juma lililopita yalishirikisha zaidi wanachama wa vyama vya upinzani, mgogoro huu unaonekana kupelekea kuwa mgogoro mkubwa zaidi wa kijamii.

Hivi sasa serikali rasmi inayoongozwa na Rais Ali Bongo, mwana wa kiongozi mbabe wa zamani Omar Bongo, inatuhumiwa kufanya udanganyifu katika uchaguzi na serikali isiyo rasmi ya upinzani. Waziri wa Mambo ya ndani wa zamani ambaye pia ni kiongozi wa upinzani André Mba Obame, amejitangaza kuwa Rais. Maandamano yaliyopangwa nchini humo yamezimwa na mamlaka kabla ya kufanyika.

Video hii kutoka kwa mtumiaji wa YouTube AfricaWeWish inaonyesha maandamano katika Chuo Kikuu Cha Omar Bongo jana:

Maasi ya Wanafunzi

Mnamo majira ya saa 8:00 Mchana tarehe 10 Februari, mwanaharakati Jean-Pierre Rougou anayesemekana kuwepo karibu na makao makuu ya serikali isiyo rasmi ya upinzani alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twita:

Gabon: révolte des étudiants de l'UOB qui refusent de vivre comme des chiens

Gabon: Machafuko kwenye Chuo Kikuu cha Omar Bongo yanafanywa na wanafunzi wanaokataa kuishi kama mbwa

Picha za maandamano ya tarehe 10 Februari zilitumwa na mkazi wa Libreville Carel Dorian Ondo Ellassoumou [fr]kwenye ukurasa wake wa Facebook:

Student protestors at the Omar Bongo University (UOB) in Libreville, Gabon on Thursday 10 February, 2011. Image from Carel Dorian Ondo Ellassoumou.

Wanafunzi wanaopinga kwenye Chuo kikuu cha Omar Bongo (UOB) mjini Libnreville, Gabon siku ya Alhamisi 10 Februari, 2011. Picha kutoka kwa Carel Dorian Ondo Ellassoumou.

The aftermath of student protests at the Omar Bongo University (UOB) in Libreville, Gabon on Thursday 10 February, 2011. Image from Carel Dorian Ondo Ellassoumou.

Matokeo ya maandamano ya kupinga kwenye Chuo kikuu cha Omar Bongo (UOB) mjini Libreville, Gabon siku ya Alhamisi 10 Februari, 2011. Picha kutoka kwa Carel Dorian Ondo Ellassoumou.

Kwa mujibu wa tovuti ya La Voix du Peuple Gabonais (Sauti ya Watu wa Gabon- LVDPG) [fr],ambayo ni gazeti la kwenye mtandao linaloendeshwa na watu wa Gabon wanaoishi ughaibuni, wanafunzi waliandamana [fr] kwa sababu hawajapokea malipo yao ya mwezi ya Euro 100 (ambazo ni sawa na Faranga za Afrika ya Kati 66,000) tangu mwezi Julai 2010.

Na pia walikuwa wakidai kurejeshwa kazini kwa maprofesa watatu, ambao wote ni wanachama wa chama cha siasa cha National Union, ambao pamoja na serikali nzima ‘isiyo rasmi’ kwa sasa ni ‘wakimbizi’ ndani ya jingo la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mjini Libreville.

LVDPG inaripotimaelezo haya kuhusu mapambano kati ya wanafunzi na mamlaka:

De violents affrontements ont par la suite éclatés entre les étudiants et les gendarmes venus les empêcher de manifester, ces derniers se permettant même de violer les franchises universitaires, car, ils seraient rentrés dans le campus et brutaliseraient les étudiants à l’intérieur de l’UOB.

Mapambano makali yalilipuka kati ya wanafunzi na askari polisi ambao walikuja ili kuwazuia wasiandamane; polisi walivunja hata kanuni za chuo kikuu, kwa sababu waliingia chuoni na kuwafanyia ukatili wanafunzi ndani ya UOB [Chuo Kikuu Cha Omar Bongo].

Waliotengeneza ukurasa wa Facebook Etudiants Gabonaisen Révolte (Wanafunzi wa Gabon katika Machafuko) [fr], ambao wanajielezea kama “wanafunzi waliokwama, wasio na wazazi wenye nguvu kwenye Chuo cha UOB” [Chuo Kikuu Cha Omar Bongo], waliandika ujumbe siku ya Alhamisi:

les forces de l ‘ordre viennent de rentrer dans l ‘université et sont en train de nous massacrer comme en 1990!!”

Majeshi ya kulinda sheria na amani yameingia chuoni na yanatuchinja, kama ilivyowahi kuwa miaka ile 1990!!”

Mwaka 1990, machafuko yaliyoanza katika Chuo Kikuu hicho hicho dhidi ya hayati Rais Omar Bongo yalizimwa bila ya huruma na mamlaka ya Gabon, yakisaidiwa na majeshi ya kigeni ya Ufaransa katika kile kilichopewa jina la “Opresheni Papa”.

Katika tukio la maandamano wiki hii, LVDPG ilionyesha taarifa ya video ambayo ilirushwa hewani kwenye idhaa ya televisheni ya Kifaransa Bfmtv.com [fr] mwaka 2009 ambayo inaonyesha hali mbaya katika Chuo Kikuu Cha Omar Bongo.

Mjibizo Kwenye Mtandao

Habari za maandamano ya wanafunzi zilitoa mwangwi katika jamii ya WaGaboni kwenye mtandao na mitazamo ikajitokeza haraka.

Akieleza hali ilivyo kuhusiana na maprofesa watatu waliofukuzwa, Paterne Sedryk Magnagaanatoa maoni kwenye ukurasa wake wa Facebook:

Comme c'est dommage! Au Gabon tu es radié de ton poste quand tu intègres un parti différent que celui du pouvoir c'est de la dictature et non la démocratie.

Aibu Gani! Nchini Gabon unaondolewa kwenye nafasi yako ukijihusisha na chama cha siasa tofauti na chama kilicho madarakani. Huu ni uongozi wa kiimla, sio demokrasi.

OK L UOB, akitoa maoni kwenye makala ya LVDPG [fr] mnamo Februari 10, anayashusha maandamano hayo:

arrete votre charabia les etudiants gabonais reclament leurs bourse rien de plus, quel revolte populaire.

Acheni kelele zenu, wanafunzi wa gabon wanataka pesa za ada tu, hakuna la zaidi, mapambano gani ya umma?

@franklinishere anaunganisha video ya bfmtv.com ya chuo kikuu kilichochakaa kwenye Twita:

#Gabon:miaka 43 ya majanga:Angalia utakachokiona kwenye Chuo Kikuu Cha Omar Bongo mjini Libreville (video ya Kifaransa): http://bit.ly/ifX0Jf

Kamata-kamata inayoendelea

Kwenye Koaci, tovuti ya habari za Kiafrika, mwanablogu anaripoti kukamatwa kwa kiongozi mwingine wa chama cha National Union huko Bitam, Kaskazini mwa Gabon:

Nous venons d’apprendre l’arrestation à Bitam (Nord du GABON) de Mr BRUNO NZE MEZUI

Tumesikia juu ya kukamatwa kwa Bw. Bruno Nze Mezui huko Bitam (Gabon Kaskazini)

LVDPG [fr] inaripoti kwamba mitaa ya upinzani mjini Libreville imezungukwa na vyombo vya utawala:

“Nous sommes pas pour venir terroriser nos populations mais plutôt assurer leur sécurité vis-à-vis des jeunes qui font le banditisme dans ces différents quartiers”, a déclaré un responsable des gendarmes.

“Hatupo hapa ili kutisha watu, bali kuhakikisha usalama wao dhidi ya vijana wanaofanya uhalifu kwenye maeneo hayo”, alisema msemaji wa polisi.”

Video inayofuata inaonyesha majeshi yalivyosambazwa huko Nkembo na Rio, maeneo ya Libreville, video hiyo ilitumwa kwenye YouTube siku ya Februari 10 na mtumiaji AfricaWeWish:

Upinzani Nchini Ufaransa Watoa Kauli

Katika makala ya blogu yenye jina “Wasikilize vijana wa Afrika”, Pascal Michelangeli, makamu Meya wa of Epinay-Sous-Seinart, mji uliopo karibu na Paris, anatofautisha msimamo wa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy juu ya mgogoro wa Tunisia na jule ambao anaonekana kuuchukua juu ya machafuko ya kisiasa nchini Gabon. Ameweka kiunganishi cha makala iliyo kwenye tovuti ya habariGabonews.gaambayo inasema kwamba Sarkozy alituma salamu kwa Ali Bongo siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake tarehe 9 Februari:

Dans ce contexte politique explosif, Nicolas Sarkozy envoyait ses voeux de joyeux anniversaire au Président Gabonais, tout en terminant sa lettre par un très distingué et laconique… « ton ami ».

Katika muktadha huu wa hali ya hatari kisiasa, Nicolas Sarkozy alituma salamu za siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Gabon, na kuhitimisha barua yake kwa maandishi yale maarufu na kwa kifupi… “rafiki yako”.

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum kuhusu Machafuko nchini Gabon 2011

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.