Vijana wa Kiyahudi na Kipalestina Watumia Video Kuuelewa Mgogoro

Mashirika mawili tofauti katika Israel na Majimbo ya Palestina yanatumia zana za video ili kuwasaidia wote, vijana wa Kiyahudi na Wakiarabu kuuelewa mgogoro na kutengeneza daraja kati yao, kwa kutengeneza nafasi ya kukutana na kuwasiliana ambamo wanaweza wakaeleza ndoto zao, yanayowagusa na mawazo yao kuhusu hali tata wanayoishi.

Moja ya miradi hiyo ni Sadaka Reut, na haya ndiyo wanayoyasema kuhusu programu yao:

Huku vijana wengi wa Kipalestina na Kiyahudi wakiwa wametengwa kimwili mmoja kutoka mwingine (kwenye jamii na shule tofauti) na hofu, ubaguzi wa rangi na mawazo potofu matokeo yake, tunatarajia kujenga namna mbadala za maingiliano kati ya makundi haya mawili. Programu ya ‘kujenga Utamaduni wa Amani’ inakusudia kutengeneza sehemu ambamo vijana wa Kipalestina na Kiyahudi wanaweza kujisikia wako sawa, wanaheshimika na kutambulika kama watu na pia kama ushirika wa kitaifa.

Wanachama wa programu hiyo pia wamekuwa wakishiriki katika mradi wa video ya Dakika Moja, ambao kwao wanajifunza kuhusu uanaharakati wa video wakati wa warsha ya wiki moja. Haya ni baadhi ya matokeo, na unaweza kuangalia yaliyobakia kwa kubonyeza ili kufikia tovuti yao:

Arab:

AM/FM:

Few love Singing:

Mradi mwingine ni Dirisha la Amani, ambao ulianza tangu mwaka 1991 kama jitihada za kutengeneza jarida la lugha na tamaduni mbili kwa ajili ya vijana kama njia ya kuwawezesha kuungana na kujifunza juu ya mgogoro, kutangaza usawa na kuwawezesha vijana. Hata hivyo, haijakuwa rahisi, kama wanavyoeleza katika tovuti yao:

“Si kazi rahisi kwa vijana wa Kipalestina na Kiyahudi kushinda idadi kubwa ya taarifa zisizo sahihi na imani potofu ambazo zinafundishwa mmoja kuhusu mwingine. Uwepo mdogo wa makutano, matokeo ya kuishi katika jamii zilizotengana na kuchochewa na mgogoro wenye machafuko mabaya ya kisiasa, vinaendeleza hofu za kihistoria, imani potofu, na chuki ambayo inawagawa jamii hizi mbili. Kwa hiyo, Dirisha (la Amani) linatilia makini kurutubisha mabadiliko makubwa katika namna ambayo vijana wa kiyahudi na Kipalestina wanavyojiona wenyewe, “wengine” pamoja na mgogoro. Washiriki wa programu za Dirisha wanapitia uzoefu ambao unatetea mabadiliko katika mgogoro kati ya jamii hizo mbili, kuelekea kwenye ukweli wa amani ambamo kila upande wanaweza kuishi. Tunaamini kuwa amani ya haki nay a kudumu ni lazima view na msingi katika maadili ya kidemokrasia, haki za binadamu, na ufahamu na kukubalika kwa “mwingine.”

Pia wanafanya kazi kwa ajili ya mradi mpya unaoitwa Kwa njia ya Lensi, ambao vijana wa umri kati ya miaka 15 mpaka 17 “waliofuzu” kutoka kwenye gazeti wanaendeleza ufundi ili kutengeneza filamu fupi fupi, habari na video nyingine nyingine ili kuendeleza “mazungumzo ya kujenga amani na maingiliano chanya yenye ufanisi.”

Hii ni video ambayo washiriki wa mradi wa Dirisha wanaongelea uzoefu wao ndani ya kikundi na jinsi walivyokabiliana na changamoto zinazojitokeza ili kujiweka nje ya uwanja waliouzoea na kuongelea mada ngumu kama vile mgogoro kati ya Israel na Palestina:

Kama watotokatika video wanavyosema kwa kutumia maneno mengi: wanaweza kuwa na wakati mgumu kukabiliana na mengi ya maoni nba mitazamo ambayo watoto wengine wanaitoa, lakini kuwa na sehemu ya kujadili masuala katika njia salama kunawasaidia kuelewa ulimwengu wanamoishi huku wakiwa na uwezekano wa kukutana, kujifunza na kushiriki na watoto wenzao pamoja na vijana na hata kubadili hiyo mitazamo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.