Habari kuhusu Wanawake na Jinsia
Asasi ya Kiraia Inayofuatilia Bunge Yawaunganisha Wabunge Wanawake na Wananchi wa Uganda
Asasi ya Kiraia ya Parliament Watch Uganda iliandaa mjadala wa kujadiliana na wabunge wanawake kwenye mtandao wa Twita kuhusu mada 'Kuwafanya Wanawake Wathaminiwe Kwenye Shughuli za Kibunge'.
Kampeni ya Facebook Yampa Mwandishi wa Iran Masih Alinejad Tuzo ya Haki za Wanawake
Mwandishi wa ki-Iran ameshinda Tuzo ya Haki za wanawake kufuatia harakati zake za kwenye mtandao wa Facebook unaoitwa "My Stealthy Freedom."
Filamu: ‘Sanaa ya Ama Ata Aidoo’
The Art of Ama Ata Aidoo ni filamu iliyotayarishwa na mtayarishaji wa filamu Yaba Badoe: The Art of Ama Ata Aidoo, inasaili mchango wa kisanii wa mmoja wa waandishi wanawake mashuhuri barani Afrika, anayeongoza kizazi hiki kwa kipaji kipya cha pekee. Dokumentari hii inasaili safari ya ubunifu ya Ama Ata...
Wanawake wa Kiislam na Kikristo Nchini Nigeria Walivyoungana Kupambana na Misimamo Mikali ya Kidini
Mchungaji Esther Ibanga kiongozi wa ki-Islam Khadija Hawaja walianzisha Mradi wa Wanawake Wasio na Mipaka miaka michache iliyopita kama jitihada za kurudisha hali ya usalama na amani katika jamii zao.
Pamoja na Wapiga Kura Kutilia Shaka Sera Zake, Croatia Yapata Rais Mwanamke
Croatia ipo katika mpasuko mkubwa wa kisiasa. Kolinda Grabar Kitarović ameweza kunyakua kiti cha uRais kufuati ushindi mwembamba alioupata dhidi ya Rais anayemaliza muda wake, Ivo Jospović katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika mwezi Januari, 2015 kwa kupata asilimia 50.74 ya kura zote.
Kuelimisha Wasichana Leo, Kuwawezesha Wanawake Kesho
Marita Seara, anayeblogu kwenye Voces Visibles (Sauti Zinazoonekana), anatukaribisha kutafakari suala la ubaguzi unaowaathiri wasichana na vijana wanaopevuka —kupata elimu– na hitaji ya kuwaelimisha wasichana wetu leo ili waweze kuwa wanawake waliowezeshwa kesho na keshokutwa. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kutetea haki za binadamu duniani Amenisty International, wasichana...
Hukumu ya Haki? Ina uzito wa Kutosha? Oscar Pistorius Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Mitano Jela
Mkimbiaji wa Afrika Kusini aliyepatwa na hatia kwa kumwuua pasipo kukusudia rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp imelinganishwa na hukumu ya jangili aliyefungwa miaka 77 jela kwa kumwuua faru mwezi Julai
Wanawake wa Kichina Waandamana Kupinga Kombe la Dunia
Offbeat China alieleza kwa nini wanawake hao wana hasira na jinsi Kombe la Dunia linavyoharibu mahusiano ya kifamilia nchini China. Wanapinga mambo mawili makubwa: 1) wapenzi wao kupuuza majukumu yao ya kifamilia kwa sababu ya kuangalia mpira usiku wa manane; 2) tabia za kucheza kamari kwa mashindano hayo.
Mambo Matano Unayopaswa kuyajua Kuhusu Harusi za Kitukimeni
Kama ulikuwa unafikiri kuchagua Turkmenistan kama nchi ya kufanyia harusi yako, unapaswa kufahamu jambo moja -linapokuja suala la kusherehekea harusi. Watukimeni huwa hawabahatishi.
Ni Rasmi Sasa, ‘Shoga’ wa Kwanza Kuteuliwa Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Nchini Puerto Rico
Wakati wengine wakina kuwa usagaji wake si suala la maana, wengine wanasisitiza kuwa hali hiyo ya kimapenzi inahusika katika kile anachokifanya kila siku.