· Disemba, 2012

Habari kuhusu Wanawake na Jinsia kutoka Disemba, 2012

Habari za Upotoshaji Kuhusu Afrika Katika Vyombo vya Habari vya Kimataifa

 Kampeni ya kumkamata #Kony2012 ilibeba mambo yaliyorahisishwa mno kuhusu Afrika. Vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe, hata hivyo, kwa sasa havina kinga dhidi ya ukosoaji wa aina hii. Hapa ni muhtasari wa watu maarufu, makosa na kutokuwepo umakini katika habari zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari vya dunia kuhusu Afrika na katika vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe

Korea Kusini: Mpango wa Kuwakutanisha Wenzi Wakwama

  26 Disemba 2012

Mpango mpya kabisa wa kuwakutanisha wenzi kwa njia rahisi katika mkesha wa Krismas nchini Korea Kusini hatimaye ulijikuta ukishindwa kabisa baada ya waliojitokeza asilimia 90 kuwa ni wanaume. Inasemekana zaidi ya watu 20,000 walijiandikisha na hata polisi walikuwepo kufuatia uwezekano wa vitendo vya ngono za kulazimisha. Mtumiaji mmoja wa mtandaoalibainisha [ko]...

Utambulisho wa Jamii ndogo ya Balkan

  23 Disemba 2012

Waandishi vijana kumi na watano kutoka katika nchi zipatazo sita tofauti wametengeneza mfululizo wa masimulizi binafsi kuhusu masuala ya namna jamii zenye watu wachache (kwa mapana yake) zinavyoweza kuwakilishwa kutoka Bosnia na Herzegovina, Kosovo, Serbia, na Macedonia. Habari zinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kijerumani, na Kifaransa katika mwonekano wa tovuti...