Habari kuhusu Wanawake na Jinsia kutoka Januari, 2010
Philippines: “Muswada wa Mkataba wa Ndoa Jadidifu”
Kikundi kimoja cha masuala maalum ya jamii nchini Philippines kinataka kuwasilisha sheria ambayo itaufanya mkataba wa ndoa kuwa na nguvu kwa miaka kumi tu. Pendekezo hilo la kipekee limezua mjadala mkali kwenye ulimwengu wa blogu.
Bolivia: Mshindi wa Zamani wa Mashindano ya Urembo Atangazwa Kugombea Ugavana wa Jimbo la Beni
Bolivia Jessica Jordan kuwa mgombea wa kiti cha ugavana kwa tiketi ya Chama Cha Ujamaa (MAS) huko kwenye jimbo la Beni, ambalo kwa kawaida hudhibitiwa na upinzani.
Georgia: Hebu Tuongelee Tendo la Ngono…
Pengine mada iliyotawala katika vyombo vya uanahabari wa kijamii vya Georgia haikuwa siasa, uchaguzi, matatizo, matetemeko ya ardhi au majanga. Badala yake, mada iliyojadiliwa sana ilikuwa inahusu kipindi kipya cha televisheni, Ghame Shorenastan. Kinachoonyeshwa kwenye Imedi TV, jina la kipindi hicho linatafsirika kama Usiku pamoja na Shorena na kinaongelea mada zinazohusu tendo la ngono.