Habari kuhusu Wanawake na Jinsia kutoka Novemba, 2013
Onesho la Mitindo Nchini Japan na Kauli Mbiu ya Kusitishwa kwa Matumizi ya Nguvu Dhidi ya Wanawake
Umoja wa Wanawake wa Asia, shirika lisilo la kimaslahi linaloshughulika na haki za wanawake linaratibu onesho la mitindo linalobeba ujumbe wa Mtindo wa Kukabiliana na Mfumo Kandamizi kwa lengo la kuvuta hisia za watu kuhusiana na suala la matumizi ya nguvu dhidi ya Wanawake.
Misri: Sabuni ya Ubikira?
Mwanaharakati wa Kimsiri Nelly Ali anashangaa: Wakati #Misri iko bize…Upuuzi kama huu uko kwenye makabati yetu ukiharibu maisha yetu "Sabuni ya Ubikira"#wanawake/a> pic.twitter.com/IXplFn2kY7 — Nelly Ali (@nellyali) November 1, 2013...
Kuwaokoa Akina Mama na Watoto Nchini Laos
Kundi la CleanBirth.org lina nia ya kuboresha hali ya huduma ya afya ya uzazi katika baadhi ya vijiji vya Laos vijijini kwa kutoa vifaa vya kuzalisha, mafunzo ya wauguzi wapya...