Hukumu ya Haki? Ina uzito wa Kutosha? Oscar Pistorius Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Mitano Jela

Paralympic athlete Oscar Pistorius in court. May 5, 2014 by Ihsaan Haffejee. Demotix.

Mkimbiaji wa Mashindano ya Paralimpiki Oscar Pistorius akiwa kizimbani. Mei 5, 2014 Imepigwa na Ihsaan Haffejee. Haki Miliki ya Demotix.

Oscar Pistorius, mkimbiaji mwenye ulemavu wa miguu wa Afrika ya Kusini alipatwa na hatia ya mauaji ya bila kukusudia kwa kumpiga risasi rafiki yake wa kike mwaka jana, amehukumiwa kifungo cha mpaka miaka mitano gerezani. Kadhalika atatumikia miaka mingine mitatu nje ya gereza kwa kosa la matumizi ya silaha kinyume cha sheria.

Pistorius anasema alidhani Reeva Steenkamp alikuwa ni kibaka aliyekuwa kaingia kwake kwa kuvunja nyumba kupitia dirisha la bafuni. Serikali, kwa mujibu wa Jaji Thokozile Masipa, ilishindwa kuthibitisha pasipo mashaka yoyote kwamba Pistorius alikusudia kumwua.

Shauri hilo, ambalo ni tukio kubwa la mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini, lililoibua hisia kubwa pamoja na ufuatiliaji mkubwa wa vyombo vya habari. Kifungo chake kimelinganisha na kifungo cha miaka 77 alichohukumiwa jangili wa faru mwezi Julai, kilichowashangaza na kuwatia hasira watumiaji wengi wa mitandao ya Twita.

Wengine wanadhani jaji alikuwa mpole sana, ushahidi wa kuharibika kwa mfumo wa haki nchini Afrika Kusini:

Hukumu ya kijinga sana. Inakejeli uhai wa mwanadamu kutoa hukumu ndogo kwa mauaji kuzidi ufisadi. Inakera

Miaka mitano? Na anaweza kutoka ndani ya miaka miwili –HAIJAKAA POA

Chini ya sheria ya Afrika Kusini, anaweza kuwa huru baada ya miezi nane tu.

Stefanie Ship aliuliza:

Nini kimeharibika kwenye dunia hii ambapo unamwua mtu na kuishia kuhukumiwa miaka mitano jela? Maisha ya mtu yana thamani ya miaka mitano?!

Kumbuka hukumu ya miaka mitano ina maana anaweza kutoka jela si zaidi ya miaka miwili

Leo hii wanawake tunajikuta maisha yetu labda hayana thamani zaidi ya nembo zinazotumika kwenye viatu vya mazoezi

Masipa unajitafutia laana bure. Hukutenda haki kwa kifo cha Steenkamps. Ni pigo kwa haki za wanawake na si haki kabisa kwa vitendo vya udhalilishaji wa majumbani (umekataa kutambua matatizo hayo kwenye hukumu yako)

Ninajua haikuwa kwa lengo la kuridhisha jamii, lakini ningependa angalau hukumu imefikia miaka kumi!

Shauri hilo haikuchukua muda mrefu kuzidi muda ambao Oscar atausotea jela

Kwenye mtandao wa Facebook, Thapelo Tips Seemise alifananisha hukumu hiyo na muda uliopita tangu mauaji ya Steenkamp yafanyike:

Ilichukua miaka miwili kufikia hitimisho la hukumu ya miaka mitano jela!!! Haki ni suala lisilowezekana nchini mwangu ‬

Wengine, hata hivyo, waliunga mkono hukumu hiyo:

Ninaunga mkono. Bado, hata hivyo miaka mitano ni nafadhali itumike kwa kuihudumia jamii, jambo ambalo nadhani ndilo Jaji alilomaanisha

Watu wnegi wana haraka ya kumhukumu Oscar utafikiri wao hawajawahi kukosea. Haya basi amehukumiwa chekeleeni na mwache kulalamika

Bila kujali vile tunavyofikiria Jaji Masipa alielewa kwa hakika lengo la hukumu. Ni kupatanisha watu sio kutafuta mkosaji

Si kila mtu anaweza kukubaliana na hukumu hiyo. Lakini Jaji Masipa alikuwa na hoja inayoeleweka kutoa hukumu

Watu muache kufanya mahitimisho hapa na kuilaani na kukejeli sheria yetu. Vinginevyo kuna uwezekano wa rufaa

Wengine walifanya hukumu hiyo iwe kichekesho:

Natarajia kuagiza toleo jipya la kitabu kinachoitwa, “Nani ya kukwepa mkono wa sheria unapoua’

Sasa…nani ananunua haki miliki ya sinema hiyo? Binafsi nadhani alama ya INAFAA KWA YEYOTE imepitiliza

Du. Kumbe ndio maana Dewani amekuja na hapa kumwuua mke wake

Shrien Dewani ni Mwingereza anayetuhumiwa kula njama kupanga mipango ya kuwezesha mke wake Anni Dewani auawe wakati wakiwa kwenye fungate nchini Afrika Kusini. Shauri lake linaendelea nchini Afrika Kusini.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.