Habari kuhusu Wanawake na Jinsia kutoka Juni, 2012
Korea ya Kusini: Mabadiliko ya Sheria kuhusu Uzazi wa Mpango Yaibua Mjadala Mkali
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya nchini Korea imetangaza kwamba dawa za kuzuia mimba za dharura zinazofahamika kama 'morning-after pills' zitaanza kupatikana kwa wingi. Hata hivyo, dawa za kuzuia mimba zisizo za dharura zimekuwa dawa za kuandikwa na daktari. Mabadiliko haya ya ghafla kuhusu dawa za kuzuia kuzaliana limeibua mjadala mkubwa mtandaoni.
Misri: Maandamano ya Kukomesha Udhalilishaji wa Kijinsia Yavamiwa
Maandamano kudai kukomeshwa kwa udhalilishaji wa kijinsia yaligeuka kuwa shubiri baada ya wanawake waliokuwa wanahusika nayo kuvamiwa na kundi la wanaume wenye hasira kwenye viwanja vya Tahrir leo(June 8, 2012). Watu walioshuhudia tukio hilo walielezea maoni yao kupitia twita.