Habari kuhusu Wanawake na Jinsia kutoka Septemba, 2012
Uganda: Binti awa Mbunge wa Kwanza Mdogo Kuliko wote Afrika
Afrika inachipuka na wanawake wa ki-Afrika wanachipuka nayo. Hivi sasa, Malawi na Liberia zinaongozwa na maraisi wanawake. Sasa nchini Uganda mbunge kinda kabisa kuliko wote barani Afrika amechaguliwa - naye ni Proscovia Alengot Oromait umri wa miaka 19 .
Pakistani: Msichana wa Kikristo wa Miaka 11 Awekwa Kizuizini kwa Kukashifu Dini.
Rimsha Masih msichana Mkristo mwenye umri wa miaka 11 ametuhumiwa kwa makosa ya kukashifu na ameshikiliwa kwa siku kumi na nne katika gereza za watoto huko Rawalpindi, nchini Pakistani. Anashitakiwa kwa kuchoma kurasa za kitabu cha Noorani Qaida, kinachotumika kwa wanafunzi wa lugha ya kiarabu, na kuziweka katika mfuko wa 'rambo'.