· Disemba, 2013

Habari kuhusu Wanawake na Jinsia kutoka Disemba, 2013

China: Mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha”

  23 Disemba 2013

Sina Weibo, tovuti ya Kichina inayofanana na Twitta, imeandaa mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha.” Picha za washindani zinaonyesha wazi kwamba wengi wao sio akina mama halisi. Hata hivyo, hizo picha zinatuambia mengi kuhusu uhusiano wa kijinsia nchini China. Soma mengine kwenye tovuti ya Offbeat China.

Taiwan: Maandamano Dhidi ya Sheria Juu ya Usawa Kwenye Ndoa

  3 Disemba 2013

Wabunge wa Yuan nchini Taiwan walipitisha muswada wa kwanza ya “Usawa kwenye Ndoa“ [zh] mnamo Oktoba 25, 2013. Novemba 30, zaidi ya watu 300,000 walipinga muswada huu, hasa dhidi ya pendekezo juu ya ndoa za jinsia moja. J. Michael Cole, mwandishi wa habari wa kujitegemea mkaazi wa Taipei, alielezea kile...

China: Jukumu la Baba

  2 Disemba 2013

Mtandao wa Offbeat China umeanzisha kipindi kipya na maarufu cha televisheni kinachojulikana kwa jina la “Baba, tunaelekea wapi?”. Kipindi hicho kinawakutanisha akina baba watano maarufu pamoja na watoto wao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali za nje kwa lengo la kushindana na bila ya uwepo wa wake zao. Hapa chini,...