Pakistani: Msichana wa Kikristo wa Miaka 11 Awekwa Kizuizini kwa Kukashifu Dini.

Msichana wa Kikristo mwenye umri wa miaka 11, Ramsha Masih amehukumiwa kwa kukashifu imani na ameshikiliwa kwa siku 14 katika gereza la watoto katika jiji pacha la mji mkuu wa Pakistani liitwalo Rawalpindi. Kuna taarifa zinazokinzana kama msichana huyu ana tatizo la ongezeko la vinasaba ama la.
Rimsha anatuhumiwa kwa kuchoma karatasi za Noorani Qaida, ambayo ni mjumuisho wa masomo ya kujifunzia kiarabu kwa wanaoanza kujifunza na kasha kuziweka ndani ya mfuko wa plastiki. Jambo hili lilitokea mnamo Agosti 16, 2012 mjini Islamabad katika mtaa wa Meherabadi katika G-12 ambao ni mtaa mdogo wenye idadi kubwa ya watu masikini na ndiyo sehemu anayoishi msichana huyu pamoja na familia yake. Kituo cha polisi cha mtaa huu kilikusanya taarifa za awali (FIR) mara baada ya mkazi jirani kumfungulia mashitaka msichana huyu.

Kosa la kukashifu imani linaelezwa katika kifungu cha sheria namba 295 cha hukumu za Pakistani ambapo mshitakiwa akikutwa na hatia anaweza kufungwa kifungo cha maisha ama hukumu ya kifo. Habari hizi zilisambazwa na mtandao wa ‘Wakristo wa Pakistani’ mnamo Agosti 18.

Habari hii ilipata umaarufu katika vyombo maarufu vya Pakistani siku tano baadae, yaani Agosti 22. Kabla ya msichana huyu kuwekwa kizuizini, baadhi ya wakazi wa mtaa anaoishi msichana huyu walizuia barabara kuu ya jiji . Kundi hili lilitaka the sheria mkononi. mwezi uliopita kundi hili lilimchoma moto mtu aliyekuwa na matatizo ya akili katika mtaa wa Bahwalpur ; ambapo mtu huyu alituhumiwa pia kwa kukashifu imani.

Waziri wa Pakistani mwenye dhamna ya usalama wa Taifa, Dkt Paul Bhatti, katika mahojiano yake na shirika la utangazaji la BBC alisema kuwa Wakristo 600 wameshayaacha makazi yao mjini Islamabad baada ya msichana huyu wa miaka 11 kuwekwa kizuizini kwa kukashifu dini. Wakristo wanaogopa kiasi cha kujificha; kumbukumbu ya mashambulizi ya Gojra ya mwaka 2009 bado wanayakumbuka pale ambapo kundi la Waislamu lilipochoma moto nyumba za wakristo na bila ya Polisi kutoa msaada wowote. Kwa mujibu wa tume ya haki za binadamu ya Pakistani, machafuko ya Gojra yalipangwa, na tena serekali ya mtaa ilihusika.
Anthony Permal ambaye ni Mpakistani mwenye asili ya Falme za Kiarabu aliwafanya watumiaji wa Twita kuipa uzito sana habari hii:

‏@anthonypermal: @anthonypermal: imethibitika- polisi wa Pakistani wamemtia nguvuni msichana wa kikristo wa miaka 11 kwa tuhuma za kukashifu dini.

Mapema hati ya makubaliano ilisambazwa kupitia mtandao kuishinikiza serikali kumlinda Rimsha asidhuriwe:

@MohsinSayeed (Mohsin Sayeed): paza sauti yako ili kumuokoa Rifta na familia yake. Kuwa na mfumo wa serikali usio wa kidini ndilo suluhisho la pekee. Kwa hakika watamuua: http://www.change.org/petitions/high-commissions-and-diplomats-of-secular-western-nations-asylum-to-the-family-of-11-year-old-christian-girl-accused-of-blasphemy#


Hati ya makubaliano ya kuishinikiza serikali
ilizitaka nchi za Magharibi zisizo za kidini kuilinda familia ya Ramsha isidhuriwe:

Wapakistani wema wanaweka saini makubaliano haya ya kuishinikiza serikali kuingilia kati jambo hili kwa sababu serikali ya Pakistani imeshindwa hata kumlinda mtawala wao mwenyewe ambaye alitokea kupinga hadharani sheria katili ya kukashifu dini ambapo mtuhumiwa anayekashifu dini atalazimika kufungwa jela na na pia hata mtuhumiwa kunyongwa.

Yapo malalamiko mengine yanayomshinikiza waziri mwenye dhamana ya kushughulikia haki za binadamu na serikali kumlinda na kumuachia huru Rimsha Masih

Wakati huohuo, raisi wa Pakistani Asif Ali Zardari aliwataka maofisa wamuwekee bayana hali halisi. Balozi wa Pakistani nchini Marekani anatwiti:

@sherryrehman: Raisi Zardari ameziwekea msisitizo mkubwa taarifa kuhusiana na kuwekwa kizuizini kwa msichana huyu wa kikristo anayetuhumiwa kukashifu dini na pia ameomba kupewa taarifa hizo..

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeitaka Pakistani kuzifanyia mabadiliko sheria zinazohusiana na kukashifu imani:

‏@amnesty (Amnesty International): Pakistani haina budi kuhakikisha kuwa msichana huyu wa kikristo aliyewekwa kizuizini baada ya kukashifu imani anakuwa salama kwani maisha yake yapo hatarinihttp://owl.li/d9aPc

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa ameitakata mamlaka ya Pakistani kumuachia huru msichana huyu. Irshad Manji, mwanamke wa kiislamu aliye mtetezi wa wanawake na mwandishi wa ‘Mungu, Uhuru wa kuishi na Upendo’ (‘Allah, Liberty and Love’) ameonesha kutokuikubali sheria ya Pakistani inayohusiana na masuala ya kukashifu imani.

‏@IrshadManji: My mahojiano yangu katika lugha ya kiingereza kuhusiana na sheria ya #Pakistani ya makosa ya kukashifu imani, ambayo ndiyo iliyopelekea msichana wa Kikristo aitwaye Rimsha kufungwa jela:

Katika mtandao wa Twita, jambo hili limeonekana kulalamikiwa na watetezi wa haki za binadamu wa Pakistani, wanaharakati pamoja na wanasiasa wachache.

‏@Ali_Abbas_Zaidi (Syed Ali Abbas Zaidi): ni habari fupi kabisa ya kusikitisha iliyokwisha wahi kuandikwa kuhusiana na sheria ya Pakistani kuhusiana na kashifa za kiimani. “Alikuwa na maika 11 tu.”

@MaheenAkhtar (Maheen Akhtar): yuko wapi Suo motto, jaji mkuu wa Pakistani, amelala ama……”

‏@beenasarwar (Beena Sarwar): Jambo la muhimu la kuzingatia kuhusiana na tuhuma hizi za kukashifu dini kuangalia nia na lengo la mtuhumiwa. Hili ndilo jambo ambalo walalamikaji wanalipuuza.. #Pakistan

Chama tawala cha PPP ( Pakistan Peoples Party) na kile cha PTI (Pakistan Tehreek Insaaf) walilaumu tukio hili. Kiongozi wa PTI, Imran Khan alitwiti:

@ImranKhanPTI: Ni aibu! Kumfunga gerezani msichana wa miaka 11 ni kinyume kabisa na imani ya kiislamu ambayo inawataka watu kuwa na huruma.

@SundasHoorain: @CMShehbaz PML_N inasubiriwa kuchukua hatua na kuonesha kutokukubaliana na kitendo hiki cha msichana wa miaka 11 kutuhumiwa kwa kukashifu imani, kupigwa na kuwekwa kizuizini #FreeRimsha

Vyama vingine vyote vya siasa vinaogopa kuzungumzia jambo hili. Jambo hili linapewa msisitizo mkubwa. Hata hivyo, hakuna mtu yeyote kutoka Pakistani anayetaka sheria hii ibatilishwe.

@anthonypermal: : hatuwezi kuikwepa sheria hii inayohusiana na kukashifu imani za wengine. Kwanza, makundi yanaweza kushinikiza mabadiliko ya sheria hii bila ya kuwa na kizuizi chochote na hivyo bila ya kuwa na wasiwasi wowote. Pili, maafisa wa polisi hawawezi kuzuia mauaji ya wazi kabisa ya washia, inawezekanaje hali hii?

Mwaka 2010, balozi Sherry Rehman aliwasilisha mabadiliko ya kifungu cha sheria ya 2010 ya makosa ya kukashifu imani kwenye mkutano mkuu wa bunge akiwa miongoni mwa wabunge wa bunge hilo. Mnamo tarehe 20, Desemba 2010, Baraza la Itikadi za Kiislamu pia ilitangaza mabadiliko yaliyopendekezwa ili kuifanya sheria hiyo isitumiwe vibaya. Lakini vyama vya kidini kama vile Jamat-i- Islami, Jamiat Ulema-e-Islam Pakistan na Sunni Tehreek pamoja na wengine vilitishia kuitisha maandamano makubwa . Baadae, Sherry Rehman alipokea vitisho vya kuuawa na hivyo kulazimika kukaa ndani ya nyumba yake bila ya kutoka.
Mapema Januari 2011, kiongozi wa Punjab, Salman Taseer alitoa maneno ya kupinga sheria za Pakistani za makosa ya kukashifu imani, hali iliyopelekea yeye kuuwawa hadharani kwa kupigwa risasi na mlinzi wake , aliyejulikana kwa jina la Mumtaz Qadri, huku ikiaminika kuwa alisukumwa kufanya mauaji haya kwa imani ya dini yake. Katika hali isiyotarajiwa Qadri naye pia amefungwa katika jela ya Adiala ambayo pia ndio jela alipofungwa Rimsha. Qadri alipokuwa anaenda kusomewa mashitaka yake, wafuasi wake walionekana wakimtupia mau waridi..

The Sunni Tehreek party rally in favor of Mumtaz Qadri, the killer of Salman Taseer, and they demand his release in Hyderabad, Pakistan. Image by Rajput Yasir. Copyright Demotix (09/01/2011)

Chama cha ki-Sunni cha Tehreek kiliwakusanya wafuasi wake ili kuanzisha mapigano katika harakati za kumtetea Muntaz Qadri, mtu aliyemuua Salman Taseer, na pia walishinikiza awekwe huru mjini Hyderabad, Pakistani.
Picha na Rajput Yasir. Haki miliki ya Demotix (09/01/2011)

Malik Siraj Akbar Katika blogu yake kwa makala ya Huffington, anasema kuwa sheria kandamizi zinazidi kuwaongezea watu wa Pakistani kutokuwa na uvumilivu wa kiimani:

Pamoja na matukio hayo ya mara kwa mara yasiyopendeza, Pakistani haipiga hatua zozote katika kuipitia upya sheria hiyo kandamizi ya kukashifu. Sheria kama hizo, kwa upande mwingine, zinawaonea waumini wa dini ndogo na, kwa upande mwingine, zikikuza zaidi kutokuvumiliana kidini katika Pakistani

Mehdi Hasan katika blogu yake anaandika kuwa:

Binafsi, sikuwahi kuelewa ni kwa nini wafuasi wengi wa dini yangu wako radhi sana kuuwa au kuwajeruhi hadi kuwaachia ulemavu wa kudumu wale ‘wanaokashifu’ Uislamu, Nabii Muhammad au Kurani. Machafuko haya yanatokana na nini? Nathubutu pia kusema, hawako imara? Je Mungu wao ni mdhaifu sana, aliye makini sana, aliye na thamani sana, kiasi cha kushindwa kuwakubali wengine?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.