Maandamano yaliyokusudia kudai kusitishwa kwa vitendo vya kubughudhiwa yaligeuka kuwa shubiri baada ya wanawake waliokuwa wanahusika nayo kushambuliwa na kikundi cha wanaume wenye hasira katika viwanja vya Tahrir leo (June 8, 2012). Watu walioshuhudia tukio hilo walielezea maoni yao kupitia twita.
Mwandishi wa habari aliyeshuhudia tukio hilo Sarah El Deeb, anaelezea kilichotokea kupitia twiti hii:
@seldeeb: Udhalilishaji kwenye maandamano hayo ulifanywa na wanaume wengi –lengo lilikuwa kuyavunja, kuwatukana na kuwadhalilisha washiriki
@seldeeb: Wanaume waliokuwa kwenye maandamano walijihami dhidi ya wavamizi lakini idadi yao ilikuwa kubwa na baadhi ya wanawake walibanwa
@seldeeb: Watu kwenye eneo la tukio walifanywa kituko na wavamizi hao na wengine wakafunga maduka yao kwa sababu ya hali kuonekana kutokuwa shwari. Mwishowe duka moja likatoa hifadhi
@seldeeb: Baadhi ya mashuhuda wanasema watu waliozunguka maandamano hayo walikuwa wakiwatukana wasichana waliokuwa wanaandamana kabla mapigano hajayaanza
Taarifa za udhalilishaji wa kijinsia zimeendelea kumiminika kwenye miezi kadhaa za maandamano. Amira Howeidy anaonyesha muktadha:
@amirahoweidy: kuwadhalilisha kijinsia waandamanaji wa kike kulivyoanza kutokea wakati wa chama cha NDP cha Mubarak tangu mwaka 2005
Turk4Syria anauliza kama kuna mtu amewekwa ndani kwa kuwadhalilisha wanawake na Mohamed Yahia anajibu:
@MohammedY: @Turk4Syria hakuna aliyekamatwa. Imepangiliwa kiufundi kiasi kwamba wengi wanahisi ghasia hizi zilianzishwa na wale walio madarakani kuwatisha waandamanaji wa kike
Sherine Thabet anapendekeza[ar]:
Na Deena Adel anahitimisha:
@deena_adel: Je, tunaweza kutumia hali hii ya kuongezeka kwa hasira baada ya udhalilishaji huu ili kuchukua hatua za kupambana nao?
Miitikio zaidi inapatikana kupitia alama hii
#EndSH kwenye mtandao wa twita.
1 maoni