Habari kuhusu Wanawake na Jinsia
Wajapani Wanajamiiana?
Ni kwa kiasi gani wajapani wanajamiana, na pia, kujamiana ndio kutasaidia kuongeza kiwango cha kuzaliana?
Muziki Wamsaidia Mwanamke wa Ki-Hindi Kujikwamua Kiuchumi
Tritha Sinah anaongoza bendi iitwayo Tritha Electric. Amekulia Kolkata na anasema muziki umekuwa njia ya kujipatia uhuru wa kifedha.
Michoro Yaonesha Harakati za Raia wa Ufilipino Wakipambana na Ukandamizaji
Nchi ya Ufilipino ina idadi ya raia wazawa wanaokadiriwa kufikia milioni 14. Wengi wa raia hawa wanaoishi maeneo ya vijijini wapo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na uharibifu unaotokana na shughuli za uchimbaji madini, harakati za utafutaji maendeleo pamoja na matumizi ya nguvu za kijeshi.
Filamu ya Difret Inayosimulia Mila ya ‘Kumteka’ Mwanamke Kulazimisha Ndoa Nchini Ethiopia
Neno "Difret" lina maana ya "ujasiri" katika lugha ya ki-Amariki. Ni filamu mpya yenye jina hilo ikisimulia mkasa wa msichana wa ki-Ethiopia aliyetekwa na wanaume waliotaka kulazimisha ndoa ya 'kimila'.
Ngono, Dini na Siasa Vinapokutana Kwenye Onesho la ‘Sidiria ya Kimalaya’
Mmarekani mwenye asili ya Pakistani Aizzah Fatima amelipa umaarufu onesho lake kwenye maeneo mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni. Jina la onesho lenyewe linaonekana kama tusi kwa wengine. Onesho linaitwa: Sidiria ya Kimalaya.
Mjamzito wa Miaka 11 Agoma Kutoa Mimba Nchini Uruguay
Niña de 11 años embarazada que no quiere abortar genera polémica➝http://t.co/uPBo6NEKcC #Aborto #Embarazo #Uruguay — Periódico La Tribuna (@PLaTribunaFunza) May 8, 2015 Kugoma kwa mjamzito wa miaka 11 kutoa mimba kumesababisha utata. Hivi karibuniTuliandika kuhusu msichana wa miaka 10 aliyekuwa mjamzito nchini Paraguay kwa kudaiwa kubakwa na baba yake wa...
Je, Utoaji wa Mimba Unaweza Kujadiliwa Kwenye Treni za Medellín?
Wakazi wa jiji la Medellín, Colombia, wanajiuliza kama treni inaweza kuwa eneo la kuzungumzia masuala ya utoaji mimba, kutokana na tangazo la kampeni ya #ladecisiónestuya (uamuzi ni wako) inayoendeshwa kwa mifumo mbalimbali ndani ya vyombo vya usafiri wa umma, hasa magari, kama inavyosimuliwa na mtumiaji wa twita aitwaye Jaime Andrés (@JAIM3_ANDR3S):...
‘Kulea Mtoto Ukiwa Mtoto': Idadi Kubwa ya Mimba za Utotoni Nchini Venezuela
Desireé Lozano, anayeblogu kwenye blogu ya Voces Visibles, anatoa mwito kwa ongezeko kubwa la mimba za utotoni nchini Venezuela, ambapo asilimia 25 ya mimba ni za vijana, na kukosekana kwa sera sahihi za kudhibiti tatizo hili na matokeo yake. Takwimu za Venezuela zinaonesha kwamba nchi hiyo ina idadi kubwa ya...
‘Msanii wa Uke’ Nchini Japani Akana Mashitaka ya Ukiukaji wa Maadili
Msanii wa Kijapani Megumi Igarashi, anayeitwa kwa jina la utani "Msanii wa uke" na vyombo vya habari vya Magharibi, anasema sanaa yake inayotokana na sehemu zake za siri haivunji maadili.
Picha za Kusikitisha za Watoto wa Kifilipino Wanaofanya Kazi Migodini
"Ni miaka minne sasa tangu nilioacha shule. Niliweza kufika darasa la sita peke yake na hapo nililazimika kuachana na masomo ili nikafanye kazi".