· Februari, 2014

Habari kuhusu Utawala kutoka Februari, 2014

Madagaska Bado Inasubiri Waziri Mkuu, Serikali Mpya

Mwezi mzima tangu Rais mteule  Hery Rajaonarimampianina achaguliwe kuwa mkuu wa nchi nchini Madagaska, bado hakuna dalili nani atakuwa waziri mkuu na akina nani wataunda serikali. Ma-Laza anahoji kuwa suala kuu si hasa nani atakuwa waziri mkuu bali atakuwa ana ajenda gani akikabidhiwa ofisi [fr]:   Un  technicien hors pair,  rassembleur,...

Rais Yanukovych wa Ukraine ang'olewa madarakani

  24 Februari 2014

Baada ya maandamano, vurugu na upinzani dhidi ya serikali uliosababisha vifo vya watu wapatao 100, Bunge la Ukraine hatimaye limepiga kura ya kumwondoa Rais Viktor Yanukovych kama hatua ya kujibu shinikizo la waandamanaji. Tayari Rais Yanukovych amenukuliwa akisema hana mpango wa kutoroka nchi. Soma zaidi kupitia kiungo hiki [en]

Pongezi kwa Waziri Mkuu Mpya wa Nepal

  23 Februari 2014

Bunge la Nepal limemchagua Bw. Sushil Koirala (75), rais wa chama cha Nepali Congress, kuwa Waziri Mkuu wa Nepal. Mwanablogu wa NNepali aishiye ughaibuni Indra anampongeza Waziri Mkuu mpya na anafikiri kwamba “zawadi aliyonayo Bw. Koirala kwa kuwawezesha wengine kwa unyenyekevu na ukweli haitaondoka wa haraka”.