Habari kuhusu Utawala kutoka Aprili, 2012
Bangladesh: Mahakama Yaamuru Kufungwa kwa Kurasa za Facebook kwa Kukashifu Dini
Mnamo tarehe 21 Machi, mahakama moja huko Bangladesh iliziamuru mamlaka zinazohusika kuzifungia kurasa tano za Facebook na tovuti moja kwa kukashifu Mtume Mohamedi, Kuruani na dini nyinginezo. Wanaharakati wa mtandaoni wana hofu kwamba kama amri hiyo itatekelezwa, basi itafungua milango kwa uhuru wa kujieleza kudhibitiwa katika siku za usoni.
Zambia: Rais Awakera Raia Waishio Nje
Rais wa Zambia, Michael Sata, amewakasirisha raia wa nchi hiyo wanaoishi ng'ambo baada ya kuwakejeli wakati wa ziara yake ya siku tatu nchini Botswana na kufifisha matumaini yao ya kuanzishwa kwa uraia wa nchi mbili katika Katiba ya nchi ya hiyo.
Mali: Raia Washtushwa na Mapinduzi ya Kijeshi
Askari walioasi wametangaza kwamba wanatwaa madaraka nchini Mali, baada ya kuwa wameteka nyara kituo cha televisheni ya taifa pamoja na ikulu. Wanadai kwamba serikali ilishindwa kuvipa vikosi vya jeshi la nchi hiyo msaada ili kuwakabili vilivyo wapiganaji wa kabila la Tuareg waliokuwa wakiteka miji ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Ukraine: Gereza la Lukyanivska – “Mahali Watu Wanapotendewa kama Wanyama”
Mnamo tarehe 2 Aprili, Televisheni ya Ukraine ya TVi ilirusha filamu iliyotayarishwa na Kostiantyn Usov kuhusu hali ya maisha na jinsi mahabusu wanavyotendewa katika gereza la Kyiv la Lukyanivska, na pia kuhusu kuenea sana kwa rushwa miongoni mwa askari magereza. Kwa uchache, wengi katika wale ambao tayari wametazama video ya Usov walishtushwa sana na yale waliyoyaona.