· Juni, 2013

Habari kuhusu Utawala kutoka Juni, 2013

Wanaharakati 36 wa Azeri Wakamatwa nchini Iran

Wanaharakati thelathini na sita wa Azeri akiwamo mwanablogu mmoja, Kiaksar, walikamatwa siku ya Alhamisi, 27 Juni katika eneo la Urmia. Vikosi vya usalama viliwaachilia huru wanaharakati hao 300 baada ya...

29 Juni 2013

Mtu Mmoja Afariki Kwenye Maandamano Yanayoitikisa Brazil

Kijana mdogo aliuawa baada ya kugongwa na gari huko Ribeirao Preto na dazeni ya watu wengine walijeruhiwa pale waandamanaji walipokuwa wakikabiliana na polisi katika majiji ya Brasilia, Rio de Janeiro na Salvador kufuatia watu zaidi ya milioni moja kujitokeza katika mitaa ya majiji makubwa na madogo nchini kote Brazil katika maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa miongo miwili.

28 Juni 2013

Iran: Utani Kuhusu Mdahalo wa Urais

Raia wa mtandaoni kadhaa walitwiti kuhusu mjadala wa pili wa rais na waliwakejeli wagombea. Potkin Azarmehr alitwiti “Wagombea urais wanaweza kuombwa kucheza muziki.”

6 Juni 2013

Wafanyakazi wa Sekta ya Afya Nchini Msumbiji Wagoma Kudai Maslahi

Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Msumbiji wamekuwa katika mgomo uliodumu kwa siku kumi na kusababisha kusimama kwa huduma katika vitengo vingi vya kutoa huduma za afya kote nchini humo. Mgogoro wao na serikali umetokana na madai yao ya kuboreshewa maslahi na mazingira ya kazi pamoja na kurekebishwa kwa gharama za chumba cha wagonjwa mahututi katika mahospitali yote nchini humo.

1 Juni 2013