Habari kuhusu Utawala kutoka Aprili, 2009
Afrika ya Kusini: ANC Yafanya Mjadala wa Uchaguzi Kwa Kutumia huduma ya Twita
Vyama vya siasa nchini Afrika ya kusini vimo katika hatua za mwisho za kampeni ya uchaguzi ujao. Chama tawala cha ANC (African National Congress) kilifanya mjadala kwa kutumia huduma ya twita.
Jamhuri Ya Kidemokrasi ya Kongo: Mahojiano na Kabila Yaamsha Gadhabu
Wanablogu wa Kikongo wakosoa mahojiano ya hivi karibuni ya rais Joseph Kabila aliyoyafanya kwenye gazeti la New York times, wanauchambua msimamo wa Kabila juu ya Rwanda, ni nani wa kulaumiwa kuhusu rushwa, na jinsi wanahabari wa Magharibi wanavyoripoti kuhusu Afrika.
Irani: Mwaka Mpya Waanza na Ujumbe Kutoka Kwa Obama
Siku Wairani waliposherehekea Norouz (Nowruz) kama sikukuu ya mwaka mpya nchini Irani, raisi wa Marekani Barak Obama alituma ujumbe kwa watu wa Irani na kwa viongozi wa Jamhuri ya kiislamu, ujumbe huo ulitoa rai ya kutaka mwanzo mpya kati ya nchi hizo mbili. Wanablogu kadhaa wametoa maoni kuhusu ujumbe huo, angalia baadhi ya maoni hayo.