Habari kuhusu Utawala kutoka Disemba, 2009
Malaysia: Mtetezi wa Uhuru wa Vyombo vya Habari Amshtaki Mwanablogu
Mwanahabari-mwanablogu mkongwe anashtakiwa katika kesi ya madai na mwanasiasa anayejulikana kwa kutetea uhuru wa habari nchini Malaysia. Angalia maoni ya wanablogu wa Malaysia.
Iran: Maandamano Tehran
Hii ni video inayoonyesha waandamanaji huko Manzarieh na Nyavaran mjini tehran wakiimba kauli mbiu dhidi ya utawala wa Kiislamu Jumamosi.
Misitu ya Madagascar Inateketezwa kwa $460,000 kwa Siku
Wakati mataifa ya dunia yanakutana huko Copenhagen kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, Madagascar, ambayo imekwishapoteza 90% ya misitu yake ya asili, inakabiliwa na tishio la biashara ya magendo ya magogo, inayotishia kuharibu kile kilichobakia katika moja ya mifumo ya mazingira yenye viumbe na mimea mingi inayotofautiana.
Misri: Makao Makuu ya Kuzimu Duniani
Wanablogu na wanaharakati wengi wa Kimisri wamekuwa wakikamatwa na Usalama wa Taifa katika nyakati tafauti kwa sababu mbalimbali –za kweli au za bandia –Wa7da Masreya aliwahoji wanablogu mbalimbali na kuweka makala ya kina kuhusu mbinu za utesaji na hila za kisaikolojia ambazo wanablogu wale wamekuwa wakikumbana nazo kwenye makao makuu ya Usalama wa Taifa katika wilaya ya Jiji la Nasr.
Urusi: Simulizi Tatu za Umaskini Uliokithiri

Mwandishi wa habari mpiga picha wa Urusi, Oleg Klimov, anatusimulia visa vitatu vya umaskini uliokithiri ambavyo alipata kusikia habari zake wakati akisubiri treni katika kituo cha treni cha Syzran, jiji lililo katika eneo la Samara la Urusi.
Iran: Maandano ya Siku ya Mwanafunzi kwenye YouTube
Maelfu ya waandamanaji hawakuujali utawala wa Kiislamu leo kwa kuandamana wakati wa siku ya mwanafunzi, wakiimba kaulimbiu dhidi ya Ali Khamenei, kiongozi wa Jamuhuri ya Kiislamu, na wakipinga sera ya mambo ya nje ya serikali.
Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni: Tafakuri ya Twita kwa Siku ya Kwanza
Wakati siku ya kwanza ya Warsha ya Pili ya Mwaka ya Wanablogu wa Uarabuni ikifungwa, tutaangalia tafakuri za washiriki kwa siku nzima, kujua wamejifunza nini na namna wanavyojisikia. Siku ilianza...
Guinea: Jaribio la Kumuua Kiongozi wa Kijeshi Dadis Camara
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kapteni Dadis Camara, kiongozi wa kikundi cha jeshi kilitwaa madaraka nchini Guinea mwezi Disemba 2008, alipigwa risasi na kujeruhiwa na mmoja wa wasaidizi wake jana mjini Conakry. Wasomaji wengi wa RFI wanaodai kuwa Camara anawajibika kwa mauaji ya waandamanaji wa upinzani yaliyotokea tarehe 28 Septemba, wanaoana kuwa haki imetendeka.
Nyenzo ya Mtandaoni ya Kufuatilia Mabadiliko ya Tabianchi
Kuelekea kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya TabiaNchi utakaofanyika Copenhagen (COP15) mwezi Desemba 2009, zifuatazo ni baadhi ya nyenzo za mtandoni za kufuatilia mabadiliko ya Tabia Nchi.