· Machi, 2014

Habari kuhusu Utawala kutoka Machi, 2014

Ufisadi Nchini Nepal: Umeanza Kuwa Tabia Inayokubalika Kijamii?

  26 Machi 2014

Watu wana hasira na wamechoka, na mashirika ya habari mara nyingi huchapisha habari kuhusu uhusiano kati ya viongozi wa kisiasa na wezi wa mali za umma lakini hakuna anayezungumzia kuingia mtaani kuandamana kupinga ufisadi -hali isiyotarajiwa kwenye nchi ambayo watu hugomea kila kisichokwenda sawa Siromani Dhungana anaandika uchambuzi kwenye blogu...

Saudi Arabia Inadhibiti Majina ya Watoto

Huruhusiwi kumwita mwanao wa kike majina kama Eman, au Sandy, au Yara. Na kama ni mvulana, majina kama Abdelnasser, Amir au Abdulmoeen hayaruhisiwi. Lakini hiyo si Saudi Arabia pekee. Kwenye mtandao wa twita, Iyad El Baghdadi anaorodhesha majina ya watoto yaliyopigwa marufuku kabisa kwenye ufalme huo: Orodha ya majina yaliyopigwa...

Maandamano ya Taiwan ya #KupingaBunge, Yatafsiriwa

  21 Machi 2014

Mamia ya watafsiri wamejipanga kupitia mtandao wa facebook kutafsiri habari kuhusu maandamano ya raia wanaojikusanya kwenye Bunge la nchi hiyo kupinga hatua ya chama tawala nchini humo kupitisha mkataba wa kibiashara wenye utata na nchi ya China.

Kwa nini Maandamano Hayatasababisha ‘Mapinduzi ya Cambodia’

  4 Machi 2014

Faine Greenwood anaandika kuhusu mhadhara wa Stanford uliotolewa na mwanaharakati wa haki za binadamu wa Cambodia Ou Virak. Aliuliza kuhusu maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea nchini Cambodia, Ou Virak alieleza kwa nini hayatasababisha ‘mapinduzi ya kisiasa': Sidhani kuwa mapinduzi ya Cambondia yatatokea, na wala sidhani yanahitajika…Hatuna hata neno muafaka kwa...

Kuumaliza Umasikini Nchini Malaysia

  4 Machi 2014

Kikundi cha Saya Anak Bangsa Malaysia kinashinikiza kupitishwa kwa Sheria ya Ujumuishi wa Kijamii ili kutatua tatizo la umasikini nchini Malaysia: Maelekezo yatokayo juu kuja chini yanaonekana kutokufanya kazi pamoja na madai tofauti ya serikali. Ili misaada ifanye kazi kweli, basi iende kupunguza ‘maumivu binafsi ya mfukoni’ kwa sababu kila...

Iran: Mwanafunzi Ahukumiwa Miaka 7 Jela

Blogu ya PersianBanoo iliripoti kuwa “mwanafunzi mwanaharakati wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Qazvin aliyefukuzwa, Maryam Shafipour amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela. Awali iliripotiwa na familia yake kuwa alikuwa amepigwa na maofisa wa kiume waliokuwa wanamhoji wakati wa kuhojiwa kukiendelea”.

Trinidad na Tobago: Kati ya Serikali Mbili

  3 Machi 2014

Katika mukhtadha wa idadi na ukubwa wa miradi inayotekelezwa kwa kupitia mipango ya serikali ya nchi hiyo, Afra Raymond anaeleza kwa nini ushirika wa kiwango cha juu unaoonyeshwa hivi sasa na Trinidad na Tobago kwa China ni “suala nyeti linalostahili tafakuri ya kina.”