Habari kuhusu Utawala kutoka Septemba, 2010
India: Marufuku Kutuma Ujumbe wa Simu za Mkononi wa Jumla
Rajesh Jain kwenye Emergic analaumu kupigwa marufuku utumaji wa jumla wa ujumbe wa simu za mkononi pamoja na ujumbe wa media-anuai ili kuzuia uhamasishaji umma kabla na baada ya hukumu...
Irani: Huenda Mwanablogu Aliyefungwa, Hossein Derakhshan (”Hoder”), Akakabiliwa na Hukumu ya Kifo
Mwendesha mashtaka huko Tehrani anataka mwanablogu wa Irani aliye gerezani Hossein Derakhshan ("Hoder") apewe adhabu ya kifo. Hakimu bado hajatoa uamuzi. Derakhshan anashtakiwa kwa kosa la “kushirikiana na dola adui, kutangeneza propaganda dhidi ya utawala wa Kiislamu, kutusi utukufu wa dini, na kutengeneza propaganda kwa ajili ya matumizi ya vikundi vinavyopinga mapinduzi." Alitiwa nguvuni miezi 22 iliyopita.
Brazil: Uchaguzi Safi kwa Mtindo wa “Jifanyie Mwenyewe”
Chini ya mwezi mmoja ujao kutakuwa na uchaguzi nchini Brazil na mradi wa Eleitor 2010 tayari umekwisha kuwa na nguvu za kubadili mchakato huo: ni mradi wa “vyanzo vya habari vya kiraia” ambao una lengo la kuratibu taarifa za raia zinazoripoti ukiukwaji wa mchakato wa uchaguzi nchini Brazil. Kwa kupitia jukwaa hilo, kuna simulisi kadhaa za kuburudisha ambazo zimeshaanza kujitokeza.