· Januari, 2009

Habari kuhusu Utawala kutoka Januari, 2009

Madagaska: Kimbunga Chasababisha Kimbunga Cha Kisiasa

  27 Januari 2009

Baada ya siku chache kupita nchini Madagaska, idadi rasmi ya madhara yaliyosababishwa na kimbunga kilichopewa jina la Fanele zimewasilishwa. Rais Ravalomanana alikwenda kwenye moja ya maeneo yaliathirika na kimbunga ili kutathmini madhara yaliyotokea. Uandishi wa kiraia wakati wa kimbunga Wakati idara inayoangalia athari na majanga, BGNRC bado haina tovuti, taarifa...

MENA: Maoni Wakati Wa Kuapishwa Obama

  26 Januari 2009

Tukio la kihistoria limetokea Marekani leo wakati Barack Obama alipoapishwa kuwa rais wa 44. Wakati kuungwa mkono kwa Obama kati ya Waarabu kumekuwa kukipungua katika miezi michache iliyopita kufuatia uteuzi wake wa baraza la mawaziri na ukimya wake kuhusu mashambulio ya Israeli huko Gaza, wanablogu wa Mashariki ya Kati na...

Malaysia: Mafunzo Yanayotokana na Mafuriko

  21 Januari 2009

Wiki iliyopita, mafuriko yaliyakumba maeneo mbalimbali katika jimbo la Sarawak nchini Malaysia. Wanablogu wanaandika yaliyotukia na mafunzo yaliyotokana na janga hilo la mafuriko. Mafuriko hayo ni mabaya zaidi kutokea katika miaka mingi nchini Malaysia.

Ugiriki: Malalamiko Kuhusu Usafirishwaji wa Silaha kuelekea Israeli

  20 Januari 2009

Wakati vita vikiendelea huko Gaza, taarifa zilizotolewa mwanzoni mwa mwezi kuhusu shehena kubwa ya silaha kutoka Marekani kuelekea Israeli kupitia bandari ya Astakos huko Ugiriki zimezua kelele kutoka kwa wanablogu wa Kigiriki. Wanablogu hao walitumia huduma ya Twita kuchunguza swala hilo na kuitia shinikizo serikali ya Ugiriki kusimamisha usafirishwaji wa silaha hizo.