Habari kuhusu Utawala kutoka Agosti, 2010
Tunisia: Picha ‘Zilizochakachuliwa’ ni Dalili ya Hali Halisi katika Vyombo vya Habari vya Kitaifa
Utumiaji vyombo vya habari vya kitaifa nchini Tunisia kama chombo vya kupigia propaganda ni jambo ambalo limeripotiwa vya kutosha. Ushahidi wa hivi karibuni kabisa wa utumiaji mbaya wa vyombo vya habari umewekwa bayana na wanablogu wa nchi hiyo mnamo tarehe 20 Agosti baada ya magazeti ya Le Temps na Assabah kuchapisha ripoti kuhusu taasisi ya hisani ya Zeitouna kutuma msaada wa kibinadamu wa chakula kwa waathirika wa mafuriko nchini Pakistani.
Irani: Kampeni ya Kutaka Mwanablogu-Mpiga Picha Hamed Saber Kuachiwa Huru
Zaidi ya wanafunzi 70 waliohitimu elimu ya chuo kikuu na wasomi wa nchini Irani wametoa wito wa kuachiwa kwa Hamed Saber, ambaye ni mwanablogu-mpiga picha na mwanasayansi wa kompyuta wa nchini humo aliyekamatwa pasipo sababu za kuelewekea mnamo tarehe 21 Juni 2010 jijini Tehran.
China: Pato la Taifa Linaongezeka, Matumizi Katika Huduma za Jamii je?
Tunaendelea kusikia kuwa uchumi wa China unaendelea kukua; je matumizi ya huduma za jamii yameongezeka? Akiba binafsi zinabaki kwenye benki, anaandika mwanablogu mmoja: kutokea hospitali mpaka shuleni mpaka malipo ya uzeeni, China haiwezi kujilinganisha.
Udhibiti Nchini Singapore
Singapore imesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo. Wanablogu wanajadili.