· Aprili, 2013

Habari kuhusu Utawala kutoka Aprili, 2013

Serikali ya Bangladeshi Yawafuatilia Wanablogu, Yawatuhumu Kuukashfu Uislam.

  28 Aprili 2013

Kadri mapambano makali kati ya wanaharakati wa Kiislamu na serikali yanavyoendelea kusababisha migongano ya kidini nchini Bangladesh, Mamlaka ya Mawasiliano ya nchi hiyo imechukua hatua ya kuwanyamazisha wanablogu wanaoonekana wapinzani wa Uislamu na serikali. Asif mshindi wa tuzo ya mwanablogu bora amekuwa akilengwa na hatua hizo kwa siku za hivi karibuni.

Jaribio la Mapinduzi katika Visiwa vya Comoro

  24 Aprili 2013

Jeshi la Pilisi nchini Comoro limesema linawashikilia watu wanaosemekana kuwa wahaini raia wa Kongo na Chadi kwa tuhuma za jaribio la kuiangusha serikali lililofanyika mwisho wa wiki. Linfo.re anaongeza kwamba [fr]: Makamanda wa Jeshi hawakutaka kupambana waziwazi na wahaini hao. Waliamini kwamba ” Kujeruhi raia wa Comoro kwa lengo la...

Asasi za Kiraia za Urusi “Zakaguliwa” na Mwendesha Mashitaka

RuNet Echo  15 Aprili 2013

Wanaharakati wa DemVybor katika jiji kuu la eneo la Voronezh waliripoti kwenye blogu ya DemVybor[ru] kwamba Asasi Zisizo ki-Serikali zinakaguliwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa jiji hilo. Mashirika manne yaliyolengwa ni wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Voronezh [ru]: ni Vuguvugu la Haki za Binadmau linaloendeshwa na...