Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Mei, 2014
Polisi wa Masedonia Wawalazimisha Waandishi Kufuta Picha za Ghasia
Ghasia, zilizofumuka baada ya kuuawa kwa kijana wa miaka 19, zilisababisha misuguano kati ya watu wenye asili ya Albania na Masedonia kwenye jiji la Skopje.
Sisi Ashinda Uchaguzi wa Rais Misri; Mpinzani Pekee Sabahi Ashika Nafasi ya Tatu
Jenerali Abdel Fattah Al-Sisi ameshinda urais kwa kishindo, huku akimbwaga mpinzani wake wa pekee Hamdeen Sabahi, ambaye ameshika nafasi ya tatu. Baada ya siku tatu za zoezi la upigaji kura, Sisi ameshinda kwa asilimia 93.3 ya kura zote. Hamdeen alipata asilimia 3 wakati asilimia 3.7 zimeharibika.
Mapigano ya Wanakijiji Kugombea Ardhi Yasababisha Maafa Nchini Madagaska
Blogu ya L'Express Mada ilitoa taarifa kwamba kijiji kizima cha Andranondambo kilichoko Kusini mwa Madagascar kiliharibiwa [fr] kufuatia mapigano ya wanakijiji yaliyosababishwa na mzozo wa kumiliki ardhi. Vita vya wenyewe...
Naijeria: Kampeni ya #Bringourgirlsback
Katikati ya mwezi Aprili, zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara kutoka shule ya sekondari iliyoko eneo la Chibok, Naijeria, kitendo kinachodaiwa kufanywa na Boko Haram, kundi la...