· Disemba, 2009

Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Disemba, 2009

Indonesia: Sarafu za Kudai Haki

Raia wa mtandaoni (Netizens) wamezindua kampeni ya kukusanya fedha zilizo katika muundo wa sarafu ili kumuunga mkono Prita Mulyasari, mama wa nyumbani raia wa Indonesia aliyeandika malalamiko yake mtandaoni dhidi ya hospitali iliyotoa huduma mbaya, na ambaye alipatikana na hatia na mahakama moja ya kosa la "kuchafua jina" la hospitali hiyo binafsi.

8 Disemba 2009

Guinea: Jaribio la Kumuua Kiongozi wa Kijeshi Dadis Camara

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kapteni Dadis Camara, kiongozi wa kikundi cha jeshi kilitwaa madaraka nchini Guinea mwezi Disemba 2008, alipigwa risasi na kujeruhiwa na mmoja wa wasaidizi wake jana mjini Conakry. Wasomaji wengi wa RFI wanaodai kuwa Camara anawajibika kwa mauaji ya waandamanaji wa upinzani yaliyotokea tarehe 28 Septemba, wanaoana kuwa haki imetendeka.

6 Disemba 2009

Urusi: Jinsi Abiria wa “Nevsky Express” Walivyoeleza Habari Kupitia Vyombo Vya Habari Vya Kijamii

Ajali ya treni la "Nevsky Express" ilitokea mbali na makazi ya watu. Ilichukua masaa kadhaa kwa wanahabari kufika kwenye eneo. Na hapo ndio picha na video za kwanza zilipoanza kuonekana kila mahali. je nini kilichotokea kwenye upashanaji habari wa kiraia ambao uliongoza njia ya kupashana habari wakati wa ajali ya ndege huko Urusi mwaka mmoja uliopita?

1 Disemba 2009