Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Februari, 2014
Nyumba ya Kiongozi wa Upinzani Nchini Zimbabwe, Tendai Biti Yalipuliwa Mara ya Pili
Biti ni katibu mkuu wa chama cha Upinzani cha MDC [Movement for Democratic Change], kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Morgan Tsvangirai.
PICHA: Vyama vya Wafanyakazi na Asasi za Kiraia Vyaandaa Mgomo
Huku ukiwa umepangiliwa ufanyike mwanzo wa kipindi cha pili cha Rais Park Geun-hye madarakani, takribani wa-Korea elfu 40 (polisi wanadai ni elfu 15) walifanya mgomo nchini kote. Mgomo huo, ulipangwa...
Madagaska Bado Inasubiri Waziri Mkuu, Serikali Mpya
Mwezi mzima tangu Rais mteule Hery Rajaonarimampianina achaguliwe kuwa mkuu wa nchi nchini Madagaska, bado hakuna dalili nani atakuwa waziri mkuu na akina nani wataunda serikali. Ma-Laza anahoji kuwa suala...
Rais Yanukovych wa Ukraine ang'olewa madarakani
Baada ya maandamano, vurugu na upinzani dhidi ya serikali uliosababisha vifo vya watu wapatao 100, Bunge la Ukraine hatimaye limepiga kura ya kumwondoa Rais Viktor Yanukovych kama hatua ya kujibu...
Upasuaji wa Kwanza wa Moyo Kongo Brazzaville
Mtandao wa kimataifa wa Afya La Chaîne de l’Espoir (Maana yake Kiungo cha Matumaini) unaripoti kuwa watoto saba wa ki-Kongo waliokuwa na hali mbaya wamenufaika na upasuaji wa moyo [fr]...
Kiongozi wa Upinzani Nchini Venezuela Leopoldo López Ajisalimisha Serikalini
Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Leopoldo López amejisalimisha mwenyewe kwa Vikosi vya Polisi, kama alivyokuwa ametangaza angefanya kwenye video [es] hiyo hapo juu. López, kiongozi wa chama cha Voluntad Popular,...
Mrembo wa Venezuela Auawa kwa Risasi Wakati Akiandamana
Genesis Carmona ameuawa kwa risasi iliyomjeruhi kichwani. Amekuwa mwathirika wa maandamano yanayoendelea nchini Venezuela.
Fuatilia Kuenea kwa Maandamano ya Ukraine
Maandamano yamechukua sura mpya tarehe 18 Februari, na Ukraine sasa imekuwa uwanja wa mapambano baina ya mamia ya maelfu ya raia na vikosi vya ulinzi.
Warusi “Wapuuza” Olimpiki na Kufuatilia Ghasia za Ukraine
Leo, baada ya ghasia na vurugu kuanza tena kwenye mitaa ya Kiev, na kugeuza kabisa upepo wa habari katika mitandao ya Kirusi. Kwa hakika, picha zinazokuja kutoka Ukraine zinaonyesha kitu kinachofanana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mwandishi wa Habari Mwingine afariki Nchini Mexico: Gregorio Jiménez de la Cruz
Kaburi la siri lilikuwa ni mwisho wa maisha ya mwandishi wa habari wa nchini Mexico, Gregorio Jiménez de la Cruz.. Waliomuua, hadi sasa bado hawajafikishwa mahakamani.