· Januari, 2011

Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Januari, 2011

Dunia ya Uarabu: “Acheni Kulia Juu Sudani”

Kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudani ya Kusini leo imeiweka nchi hiyo kwenye uangalizi wa karibu miongoni mwa watumiaji wa twita wa Kiarabu. Kuanzia Saudi Arabia mpaka Palestina, watumiaji Twita wa Kiarabu wanajadiliana kuhusu mshikamano, kugawanyika na rasili mali za Sudani.

31 Januari 2011

Sudani: Kura ya Maoni ya Sudani ya Kusini katika Picha

Kura ya maoni inaendelea kupigwa huko Kusini mwa Sudani tangu tarehe 9 mpaka 15 Januari 2011 kuamua iwapo sehemu hiyo ya kusini itaendelea kubaki kuwa sehemu ya Sudani ama iwe nchi huru inayojitegemea. Hizi ni picha zinazoweka kumbukumbu muhimu ya kihistoria ya kura hiyo ya maoni katika Sudani ya Kusini.

28 Januari 2011

Tunisia: Anonymous Dhidi ya Ammar – Nani Atashinda Vita ya Kuchuja Habari?

Kichuja habari cha Tunisia, kinachojulikana kama Ammar, kinaeendelea kutishia kuziharibu na kuzifunga anuani za wanaharakati wa mtandaoni, katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikishuhudia wimbi la maandamano tangu katikati ya mwezi Desemba. Ni leo tu, wanaharakati wamedai kwamba serikali imeingilia anuani zao za barua pepe,na kuziingilia blogu na mitandao yao ya kijamii, na kuzizuia zisifanye kazi. Hatua hii inaonekana kuja kama kulipiza kisasi kwa shambulio lililofanywa na kikundi cha wanaharakati wa mtanda0ni wanaojulikana kama Anonymous, ambalo lililenga njia na mitandao ya muhimu ya Serikali ya Tunisia.

24 Januari 2011