· Mei, 2013

Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Mei, 2013

Msumbiji: Madaktari Watangaza Mgomo

Madaktari nchini Msumbiji wametangaza rasmi kuwa wanaingia kwenye mgomo. Wanadhani “walikandamizwa, kutukanwa na kunyanyaswa” katika mkutano wao wa mwisho na serikali. Mgomo huu wa sasa unafuatia mgomo wa madaktari uliofanyika...

20 Mei 2013

Mwanamke Aokolewa Kwenye Kifusi Baada ya Siku 17

Siku ifananayo na ile iliyogharimu maisha ya watu mara baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa tisa huko Savar pembezoni mwa mji mkuu wa Banglasesh, Dhaka, idadi ya watu waliofariki imeongezeka hadi 1,055 , idadi inayopelekea tukio hili kuwa tukio lililowahi kuua watu wengi zaidi tokea lile la tarehe 9/11 kulipotokea mashambulizi ya kigaidi, mfanyakazi mwanamke ajulikanaye kwa jina la Reshma Begum amekutwa akiwa hai mara baada ya kuzuiwa na kifusi cha jengo hilo kwa siku 17.

15 Mei 2013

Pakistan: Imran Khan Aanguka na Kuumia Akiwa Kwenye Jukwaa la Kampeni

Aliyekuwa mchezaji maarufu wa kriketi na kisha kuamua kuwa mwanasiasa, ambaye kampeni yake ina tumaini kubwa la kuleta "Pakistan Mpya" aliyeweza kushawishi idadi kubwa ya vijana pamoja na wapiga kura wanaotokea mijini katika mikutano yake, alivunjika vifupa vitatu vya uti wa mgongo pamoja na mbavu baada ya kuanguka kutoka kwenye winchi iliyokuwa katika kimo cha futi 15 mda mfupi kabla ya kuhutubia. tukio hili limeonekana kuliunganisha tena taifa hili lililojigawa kwa visasi vinavyotokana na uchaguzi utakaofanyika mapema wiki hii.

11 Mei 2013