Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Juni, 2013
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Nchini Saudi Afungwa Miaka Nane Jela
Abdulkareem al-Khadar, mwanafamilia ya kifalme mwanzilishi wa shirika la haki za binadamu, Chama cha ki-Saudi cha Haki za Kiraia na Kisiasa (ACPRA), alihukumiwa kifungo cha miaka nane jela kwa kosa la uchochezi na kuanzisha shirika la haki za binadamu lisilo na leseni pamoja na mashtaka mengine
PICHA: Mamia Wakamatwa Nchini Brazil kwa Kupinga Ongezeko la Nauli za Mabasi
Polisi wanakabiliana kwa vurugu na kwa kutumia moshi wa machozi dhidi ya waandamanaji wanaopinga ongezeko la nauli ya usafiri wa umma katika maandamano ya yalioyodumu kwa siku ya nne mfululizo huko Sao Paulo. Maandamano haya ni sehemu ya Harakati za Kudai Usafiri wa Bure ambazo tayari zimeshasambaa katika miji mikuu mingine yote nchini Brazil.
Kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari wa Kimasedonia Kwachochea Maandamano
Waandishi wa habari wa Kimasedonia walikusanyika [tazama video na soma nakala] mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai hivi leo katika mji mkuu Skopje kupinga kukamatwa kwa mwenzao, Tomislav Kezarovski, kwa mujibu wa...