Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Mei, 2011
Msumbiji: Polisi Washambulia Waandamanaji
Siku ya tarehe 6 Aprili, maofisa wa tawi la Polisi wa jamhuri ya msumbiji (PRM) – Kikosi cha Askari Maalum wa Dharura (FIR) – walitumia nguvukusitisha maandamano ya wafanyakazi wa shirika binafsi la ulinzi Group Four Security (G4S). Kwenye Facebook, wanamtandao walionesha kuchukizwa kwao kutokana na vitendo hivyo vya kikatili na kuhoji wajibu wa polisi, sheria na haki za binadamu.