Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Septemba, 2014
Waandamanaji Wanaodai Demokrasia Wageuza Hong Kong Kuwa Bahari ya Miamvuli
Yakiwa yamepewa jina la utani la "mapinduzi ya miamvuli" na baadhi ya vyombo vya habari, maandamano ya Hong Kong yatawaliwa na waandamanaji wanaojikinga na mabomu ya kutoa machozi kwa kutumia miamvuli.
Polisi wa Hong Kong Wawapiga Mabomu ya Machozi Waandamanaji Wanaodai Demokrasia
Polisi walipambana na waandamanaji baada ya maandamano ya kukaa katikati ya jiji la Hong Kong kudai uchaguzi wa demekrasia halisi.
Video ya Kuonesha namna Mlima Ontake Ulivyolipuka
Mtu mmoja amethibitika kufa, wakati wengine wapatao hamsini wakiwa wamejeruhiwa vibaya, na wengine kumi hawajulikani walipo baada ya Mlima Ontake, ulio maarufu kwa ukweaji mlima, katikati ya Japani, kulipuka
ISIS Yaonesha Video ya Mauaji ya Mwandishi Steven Sotloff
Video ya dakika tatu inayodaiwa kuonesha kuuawa kwa kukatwa kichwa kwa Steven Sotloff, ambaye amekuwa akifanya kazi katika maeneo hatarishi ya Mashariki ya Kati yakiwemo ya nchi za Bahrain, Syria, Egypt, Libya na Uturuki.
Nzige Wavamia Mji Mkuu wa Madagaska
#valala pic.twitter.com/YHzOx5Q8QU — Vaintche Rahouli (@vincraholi) Agosti 28, 2014 Watumiaji-mtandao wa Twita na Facebook kutoka mji mkuu wa Madagaska, Antananarivo, wamepachika picha kadhaa za nzige wakivamia mji. Uvamizi wa nzige...
Watu 12 Hufa na Waniger 27,000 Huachwa Bila Makazi Kutokana na Mafuriko
Mvua kubwa na mafuriko nchini Niger yamewaua watu 12 na kuacha maelfu bila makazi. Mito katika Niamey na maeneo ya karibu imefurika na kuharibu maelfu ya nyumba. Katika kanda, uharibifu wa...