Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Agosti, 2012
Ufilipino: Mafuriko Yaathiri Vitongoji vya Jiji la Manila na Mikoa ya Karibu
Mvua kubwa ilisababisha mafuriko katika vitongoji vingi ya jiji la Manila pamoja na majimbo ya jirani katika Kisiwa cha Luzon nchini Ufilipino. Mhariri wa Global Voices aliye huko Manila, Mong Palatino, anakusanya picha kutoka katika majukwaa mbalimbali ya habari za kiraia yanayoonyesha athari kubwa ya mafuriko hayo katika mji huo mkuu wa nchi.
Saudi Arabia: Mwanaharakati Reema Al Joresh Atiwa Kizuizini katika Sikukuu ya Idi
"Hamjambo? Polisi wamenikamata mimi na watoto wangu." - Reema Al Joresh, mke wa mfungwa ambaye amekuwa kizuizini kwa miaka nane bila kufunguliwa mashtaka, alikuwa akielekea msikitini ili kutoa zawazi 500 pamoja na barua ya kueneza taarifa kuhusu itiaji nguvuni wa kiholela katika ufalme huo.