Naijeria: Kampeni ya #Bringourgirlsback

 


Bango la kampeni. Wasichana 234 wenye umri kati ya miaka 16-18 walitekwa nyara takribani wiki mbili zilizopita nchini Naijeria: #bringourgirlsback. Chanzo: Ukurasa wa Facebook #bringourgirlsback ‬- Kwa Matumizi ya Umma

Katikati ya mwezi Aprili, zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara kutoka shule ya sekondari iliyoko eneo la Chibok, Naijeria, kitendo kinachodaiwa kufanywa na Boko Haram, kundi la kigaidi lililoko katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Ingawa baadhi ya wasichana 57 wameweza kutoroka, bado wengine wengi wako mikononi mwa watekaji nyara. Tarehe Aprili 30, wanawake Wanaijeria waliandaa maandamano katika miji kote nchini Naijeria kushurutisha serikali iongeze jitihada zake za kuwaokoa wasichana hao. Tovuti ya Waandishi wa Habari ya Sahara ilichapisha picha kutoka Kaduna, Nigeria. Wanablogu Wanaijeria pia walifungua ukurasa wa mtandao wa Facebook wakitumia alama ashiria #bringourgirlsback kutoa wito wa kueneza hasira kwenye mtandao dhidi ya hatua hii ya jinai ya waasi wenye msimamo mkali.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.